MBEYA CITY YAITANDIKA BAO 2 – 1 SIMBA KATIKA LIGI KUU YA TANZANIA BARA
Katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyopigwa katika
uwanja wa Taifa leo, wekundu wa Msimbazi Simba wamejikuta wakivutwa
sharubu baada ya kuchezea kichapo cha bao 2 – 1 dhidi ya Mbeya City ya
jijini Mbeya.
Timu ya Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza
kupitia mchezaji wake, Ibrahim Ajib, hata hivyo Simba walionekana
kupwaya hivyo kutoa nafasi kwa Mbeya City kuongeza mashambulizi hivyo
kupata bao la kusawazisha mnamo dakika ya 77 kutoka kwa mchezaji wao
Kibopole.
Mbeya City ilipata bao la pili na la ushindi kwa njia ya
mkwaju wa penalti baada ya mlinda mlango wa Simba, Peter Manyika
kumuangusha mchezaji wa Mbeya City na mchezo kumalizika kwa Mbeya City
kushinda 2 – 1 dhidi ya Simba.
MBEYA CITY YAITANDIKA BAO 2 – 1 SIMBA KATIKA LIGI KUU YA TANZANIA BARA
Reviewed by crispaseve
on
01:34
Rating:
Post a Comment