LIL WAYNE KUWACHUKUA DRAKE NA NICKI MINAJ KUTOKA CASH MONEY
Rapa Lil Wayne ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka
kuihama lebo ya Cash money inayomilikiwa na Birdman na kuongeza kwamba
ataondoka na marapa wenzake ambao ni Drake pamoja na Nicki Minaj.
Wayne ambaye ni C.E.O wa Young Money, amepanga kumshtaki
Birdman kwa kitendo cha kutotaka kumuachia katika lebo yake sambamba na
madai ya dola za kimarekani milioni 8 kama sehemu ya malipo ya awali kwa
ajili ya albamu yake mpya ya The Carter V ambayo bado haijatoka.
Aidha Rapa huyo amedai atahakikisha wasanii wote wa Young
Money wanakuwa chini yake kwa sababu mikataba yao iko chini ya lebo
yake.
Hata katika remix ya wimbo wake wa Coco unaopatika katika mixtape yake mpya ”Sorry 4 the wait 2”, Wayne anasema, ”I Ain’t trippin’, I got Barbie, I got Drake too”. Akiamini kwamba Drake na Nicki hawatoweza kumsaliti.
LIL WAYNE KUWACHUKUA DRAKE NA NICKI MINAJ KUTOKA CASH MONEY
Reviewed by crispaseve
on
01:33
Rating:
Post a Comment