MSANII WA MAREKANI SUGE KNIGHT AKAMATWA KWA MAUAJI
Msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight.
Polisi nchini Los Angeles inasema
kuwa msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani Marion Suge Knight
amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na
gari lake hadi kumuua na baadaye kutoroka.
Polisi wanasema kuwa Knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwengine akijeruhiwa vibaya.
Wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.
Suge Knight ni mwanzilishi wa kampuni ya Death Row Records ambayo iliwazindua wasanii maarufu wa mziki wa rap akiwemo Snoop Dogg na marehemu Tupac Shakur.
MSANII WA MAREKANI SUGE KNIGHT AKAMATWA KWA MAUAJI
Reviewed by crispaseve
on
21:58
Rating:
Post a Comment