MTOTO WA JACKIE CHAN AFUNGWA JELA MIEZI SITA HUKO CHINA
Mtoto wa mwigizaji maarufu nchini China, Jackie Chan,
Jaycee Chan amekutwa na hatia na kufungwa miezi sita gerezani kwa kosa
la kutoa hifadhi na kuwaficha watuhumiwa wa dawa za kulevya nchini humo.

Jackie Chan(Kulia) na kijana wake wa kiume Jaycee(Kushoto)
Hukumu hiyo iliyotolewa katika mahakama ya jijini Beijing
kufuatia sheria kali juu ya matumizi yasiyo halali ya madawa ya kulevya.
Jaycee mwenye miaka 32 aliwekwa kizuizini mwezi Agosti mwaka
jana baada ya polisi nchini humo kugundua kiasi cha zaidi ya gramu 100
za bangi zikiwa nyumbani kwake.
Jaycee alikiri kosa na kusema ukweli kwa polisi mara tuu
walipofika nyumbani kwake kwa sababu hakujua jinsi ya kukabiliana na
masuala ya bangi na madawa ya kulevya.
Kukiri makosa kwa mtoto huyo wa muigizaji maarufu Dunia,
inatoa ujumbe muhimu kwa serikali ya China kuwa hakuna mtu yeyote mwenye
kinga juu ya sheria kali dhidi ya madawa ya kulevya nchini humo
iliyoanza kutumika rasmi Juni mwaka 2014.
Mbali na kifungo hicho cha miezi sita, Jaycee pia atatozwa faini ya kiasi cha dola za kimarekani 322 kwa kosa hilo.
Baba yake ambaye aliyeuliwa na polisi wa China kuwa balozi wa
kudhibiti mihadarati mwaka 2009, amesema kuwa kijana wake huyo amempa
aibu na kumuhuzunisha kwa tukio hilo.
MTOTO WA JACKIE CHAN AFUNGWA JELA MIEZI SITA HUKO CHINA
Reviewed by crispaseve
on
22:24
Rating:

Post a Comment