Waimbaji wataka nafasi zaidi Tamasha la Pasaka
Na Samia Mussa.
WAKATI
wakazi wa mikoa kadhaa hapa nchini wakiomba Tamasha la Pasaka lipite kwenye
mikoa yao, baadhi ya waimbaji wakongwe wa tamasha hilo linalotimiza miaka 15
tangu kuanzishwa kwake, wametoa
mapendekezo yao kwa wandaaji Kampuni ya Msama Promotions.
Wakizungumza
hivi karibuni waimbaji hao, walianza kwa kuipongeza Kampuni
hiyo kufikisha miaka hiyo bila kutetereka huku wakitoa mapendekezo mbalimbali
yatakayoboresha zaidi matamasha yajayo.
Moja
ya mapendekezo hayo ni pamoja na kutaka kila mwimbaji apate nafasi angalau ya kuimba nyimbo mbili ukizingatia
waimbaji hao wana albamu zaidi ya tatu jambo ambalo kwao linawapa ugumu kwao
pamoja na mashabiki.
Hayo
alisemwa na mwimbaji nguli Upendo Nkone ambapo alisema licha ya kampuni hiyo
kujitahidi kufanya vizuri ikiwa pamoja na kuimba kwa kutumia vyombo hivyo Kamati
ya Maandalizi inatakiwa kubadilisha vitu vichache ikiwemo kupewa dakika za
kuimba kama wanavyofanya nchi zilizoendelea si moja kama ilivyozoeleka.
Waimbaji wataka nafasi zaidi Tamasha la Pasaka
Reviewed by crispaseve
on
07:44
Rating:
Post a Comment