ARSENAL YAANGUSHA KARAMU NZITO, YAIFYATUA ASTON VILLA 5-0
Arsenal
imezidi kucharuka kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuichakaza Aston
Villa 5-0 katika mechi ya kutakata iliyochezwa Emirates Stadium.
Ikicheza bila mshambuliaji wake tegemeo Alexis Sanchez, Arsenal ikatandaza soka maridadi na kupata bao la mapema kupitia kwa Olivier Giroud kunako dakika ya nane.
Ni kipindi cha pili ndicho kilichokuwa na maangamizi kwa Aston Villa ambapo Arsenal ilisukumiza mabao manne wavuni kupitia kwa Ozil, Walcott, Cazorla na Bellerin.
Ozil akifunga bao la pili
Waclott akitupia goli la tatu
Cazorla anaifungia Arsenal bao la nne kwa penalti
Hector Bellerin akihitimisha karamu ya magoli kwa bao la tano
Arsenal
(4-2-3-1): Ospina 7; Bellerin 7.5, Mertesacker 7, Kosceilny 7, Monreal
7; Coquelin 7.5, Aaron Ramsey 7 (Flamini 77, 6.5), Theo Walcott 7
(Rosicky 70, 6.5), Santi Cazorla 9, Mesut Ozil 8.5; Olivier Giroud
(Akpom 70, 7).
Aston Villa (4-3-3): Guzan 6.5; Hutton 5.5, Clark 5.5, Okore 5.5, Richardson 6; Sanchez 4 (Westwood 76, 5), Delph 6, Cleverley 5 (Agbonlahor 66, 5); Gil 6, Weimann 5.5 (Sinclair 66, 5), Benteke 6
ARSENAL YAANGUSHA KARAMU NZITO, YAIFYATUA ASTON VILLA 5-0
Reviewed by crispaseve
on
10:19
Rating:
Post a Comment