JAHAZI MODERN TAARAB NA MASHUJAA BAND KUONYESHANA UFUNDI LEO USIKU TRAVERTINE HOTEL MAGOMENI
Onyesho
lililokuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Jahazi Modern Taarab na
Mashujaa Band limewadia na kilichobakia ni kila bendi kuonyesha ufundi
wake jukwaani.
Ni
Jumapili ya leo ndani ya Travertine Hotel, ambapo wakali wa tuzo za
taraab Jahazi Modern Taarab watakutana jukwaa moja na wakali wa tuzo za
dansi Mashujaa Band.
Kwa
muda wa miaka miwili mfululizo Jahazi na Mashujaa wamekuwa wakizitawala
tuzo za Kilimanjaro (KTMA) kwa upande wa taarab na dansi na sasa
makundi hayo mawili yameamua kukutana jukwaa moja kuonyeshana ufundi.
Mratibu
wa onyesho hilo, Seif Magwaru ameiambia Saluti5 kuwa hilo ni tukio la
kihistoria, ni usiku wa wakali wa tuzo za kili kwa taarab na dansi,
hivyo si kitu cha kukosa
JAHAZI MODERN TAARAB NA MASHUJAA BAND KUONYESHANA UFUNDI LEO USIKU TRAVERTINE HOTEL MAGOMENI
Reviewed by crispaseve
on
10:24
Rating:
Post a Comment