KAMPUNI YA TRUMARK YAANDAA WARSHA MAALUMU KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ITAKAYOFANYIKA MACHI, 7, 2015 MLIMANI CITY DAR ES SALAAM
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo (kulia), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu warsha
maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 7, 2015 ukumbi wa Mlimani City.
Wengine kutoka kushoto ni maofisa wa Trumark, Antu Mandoza na Nuru Lyau.
Mratibu wa Warsha hiyo Antu Mandoza (kulia), akisisitiza
jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa warsha hiyo, Nuru Lyau.
Ofisa wa Kampuni ya Trumark, Zulekha Samwix (kulia), akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya TruMark ya jijini Dar es Salaam imeandaa warsha yenye lengo la
kumjengea mwanamke uwezo wa kutambua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.
Hayo
yamemwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,
Agness Mgongo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Mgongo
alisema warsha hiyo itafanyika Machi 7, 2015 katika ukumbi wa mikutano
wa Mlimani City ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani.
‘Tunataka
tumjengee mwanamke uwezo wa kujiamini, kujithamini na kutambua kuwa
changamoto anazozipata ni fursa zitakazomfanya aweze kupambana na makali
ya maisha na kisha kujiendeleza bila kumtegemea mwanaume’ alisema
Mgongo.
Aidha
Mgongo alisema kuwa warsha hiyo itajumuisha shuhuda na maonesho ya
bidhaa na kazi za mikono kutoka kwa wanawake waliofanikiwa kupitia
changamoto mbalimbali walizozipitia.‘Siwezi
kuwataja ila watakuwepo wanawake ambao walikumbwa na changamoto
mbalimbali lakini hawakukata tamaa na mwisho wa siku wakafanikiwa,’
alisema Mgongo.
Naye
kwa upande wake Mratibu Mkuu wa warsha hiyo, Antu Mandoza alisema kuwa
kutakuwa na kiingilio cha sh. 50,000 ambayo asilimia 10 ya fedha
zitazopatikana zitaelekezwa katika kuwaandaa wasichana kujitambua mapema
kabla ya kuingia katika soko la ajira.
‘Tutaenda
katika shule mbalimbali za wasichana kuwafundisha mbinu nbalimbali za
kuwa wajasiriamali na kujiajiri punde wanapohitimu masomo yao’ alisema
Mandoza.
KAMPUNI YA TRUMARK YAANDAA WARSHA MAALUMU KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ITAKAYOFANYIKA MACHI, 7, 2015 MLIMANI CITY DAR ES SALAAM
Reviewed by crispaseve
on
01:33
Rating:
Post a Comment