Header AD

KITUO CHA RADIO 5 WAADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI

SAM_1097
Kushoto ni Mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip na Ashura Mohamed wakiwa katika picha ya  pamoja na wanafunzi wa sekondari walioshiriki katika maadhimisho hayo ya Radio duniani.
 
Akizungumza na waandishi wahabari hivi karibuni Mkuu wa vipindi wa Radio 5 Bw.Mathew Philip alisema maadhimisho hayo yalidhaminiwa na kituo hicho pamoja na Farm Radio, ikiwa ni kuhadhimisha siku ya Radio duniani ambapo ilifanyika  tarehe 13/2/2015 jijini Arusha.
 
Bw.Mathew alisema kuwa wakulima pamoja navijana wa kanda ya kaskazini wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari,walipatana  fursa ya kutembelea kituo hicho na kuona namna inavyoendesha vipindi vyake ikiwemo kipindi cha afya ya akili kwa vijana(Positive mood),Fahari yangu kipindi kinacho wagusa wakulima 
 
Alitoa wito kwa Radio zingine kuwa na utaratibu wa kuhadhimisha siku hiyo kwa kuwa itasaidia kuongeza uaminifu mkubwa na wasikilizaji kwa ujumla
Kwa upande wake Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusisitiza jamii kusikiliza radio hasa vipindi vya elimishi vinavyopatikana katika vituo vya radio hapa nchini na Afrika.
 
Aidha alisema kuwa Jamii hasa wakulima wakisikiliza radio watapata elimu na taarifa mbalimbali za kile wanachokiitaji kwa wakati sahihi ikiwemo taarifa za hali ya hewa.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
SAM_1092
Wakulima pamoja na vijana kanda ya kaskazini wakiwa katika majadiliano mara baada ya kufanya ziara katika kituo cha Radio 5 nakuona namna inavyoendesha vipindi vyake katika maadhimisho siku ya radio duniani iliyofanyika 13/2/2015 jijini Arusha.
SAM_1093
Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip akiteta jambo na mkulima aliyefika katika maadhimisho hayo.
KITUO CHA RADIO 5 WAADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI KITUO CHA RADIO 5 WAADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI Reviewed by crispaseve on 07:31 Rating: 5

No comments

Post AD