Kumekucha ‘Chicken Wings Bonanza & Family Day Out’ Kufanyika Feb 28
Na Andrew Chale wa modewji blog
Bonanza
kubwa la Nyama ya kuku ‘’Chicken Wings’ litakalokutanisha watu
mbalimbali wakiwemo marafiki na familia mbalimbali linatarajia kufanyika
Februari 28, ndani ya Azura Beach Club, Kawe, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jaunt Africa Ltd,
Acquiline Mlulla waandaji wa Bonanza hilo la ‘Chicken Wings Bonanza
& Family Out’ linalotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza, Alisema
tayari maandalizi yamekamilika na watu mbalimbali wameombwa kujitokeza
kwa wingi ikiwemo na familia zao kufurahia siku hiyo muhimu na familia
zao na kufurahia Nyama ya kuku.
“Bonanza
la ‘Chicken Wings, ni la kipekee kwani si la kukosa kabisa hiyo
Februari 28, kwa kiingilio cha sh 10,000 kwa watu wazima na sh 4,000
kwa watoto. Ambapo milango itakuwa wazi kuanzia saa nne asubuhi tiketi
zitakatishiwa hapo hapo huku saa sita mchana likianza rasmi na
kuendelea hadi usiku.
Familia
na watu wote wataburudika, watafurahia nyama ya kuku zitakazoandaliwa
kwa utaalamu wa hali juu pamoja na shamra shamra mbalimbali na muziki na
matukio ya ‘surprise’ kwa kila atakayefika” alieleza Acquiline Mlulla.
Acquline
Mlulla alibainisha kuwa, Bonanza hilo litakuwa la kipekee kwa hapa
nchini, kwani pia litakuwa na michezo ya ufukweni ikiwemo Beach Soccer,
swimming pool, pamoja na madansa maalum watakaokuwa wakitoa burudani
kutoka kwa Ma-dj wakubwa wa Bongo.
Bonanaza
hilo limedhaminiwa na Jaunt Africa Ltd, Dodoma Wine, Hot Spot Magazine,
Coca- Cola, Michuzi Media Group na wengine wengi.
For updates or to find out more about CHICKEN WINGS BONANZA or to request a sponsorship details, please contact us at: +255 755 048 362 or +255 658 289 737 Email: info@jaunt-africa.com or SKPE: acquiline.mlulla
Kumekucha ‘Chicken Wings Bonanza & Family Day Out’ Kufanyika Feb 28
Reviewed by crispaseve
on
06:40
Rating:
Post a Comment