Mh. Shyrose Bhanji mgeni rasmi usiku wa Lady in Red 2015
..Kufanyika Nyumbani Lounge Ijumaa Februari 13
Na Andrew Chale.
Mwaka huu ni wa 11, tokea kuanzishwa kwa Lady in red, ambapo itajumuisha wanamitindo
mbalimbali pamoja na wabunifu tofauti katika redcapert iliyotayarishwa maalum
kwa ajili ya usiku huo.Kwa mujibu wa wandaaji wa Usiku huo wa Lady in red 2015,
Asia Idarous Khamsin ‘Mama wa Mitindo’
akishirikiana na Fashionnews
Tanzania, alieleza kuwa usiku huo utapambwa na Gusa Gusa Min Band, kundil la Ngoma za asili na wengineo.
“Ijumaa ya Februari
13 ni siku maalum ya usiku wa Lady in red. Kwa kiingilio cha sh 10,000 kawaida
na sh. 20,000 kwa upande wa V.I.P. Nguo nyekundu za Valentine day zitauzwa
sambamba na kufurahia burudani
mbalimbali” alisema Asia Idarous na kuongeza kuwa vazi maalum la usiku huo ni
rangi nyekundu na tiketi za usiku zinapatikana Fabak fashions, Mikocheni kwa
Mwalimu Nyerere na Kobaz shop, Nyumbani Lounge.
Aidha, usiku huo wa Lady in red 2015, mdhamini mkuu ni Maji Poa, wengine ni
Darling hair, , Vayle Spring, Eventlite,
michuzi media group, chaneli ten, magic fm, sibuka tv, profile and style, Jambo
Leo, mashughuli blog, vijimambo blog,
Voice of America, Mo blog, Supernewstz blog na wengine wengi.
Mh. Shyrose Bhanji mgeni rasmi usiku wa Lady in Red 2015
Reviewed by crispaseve
on
09:07
Rating:
Post a Comment