Header AD

TWANGA PEPETA KUFANYA ONYESHO MAALUM LA VALENTINE DAY.

 
BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa kesho itafanya onyesho maalum ya kusherekea siku ya wapendanao ‘Valentine Day’, kwenye ukumbi wao wa nyunmbi Mango Garden, Kinondoni.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka amesema kuwa pia onyesho hilo watatambulisha nyimbo zao mpya zilizoko kwenye chati. Pia mkurugenzi huyo alisema kuwa bendi hiyo itapiga nyimbo zao zote za zamani zilizovuma wakati huo. Aliwataka mashabiki wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria onyesho la aina yake ambalo  litabubikwa na zawadi kibao za Valentine.

“Tumejianda vizuri kwa onyesho la Valentine. Onyesho hili limeboreshwa zaidi ya lile la kumpongeza mwanamuziki wao kongwe Lwiza Mbutu lililofanyika wiki iliyopita ambalo iliudhuriwa na umati wa mashabiki,” alisema Asha.

“Tunaomba watu wajitokeze kwa wingi waje waangalie onyesho letu  maalum  kwani ukizingatia kwamba Valentine Day hufanyika mara moja kwa mwaka,” alisema Asha. Naye mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika kilichobaki ni muda kufika ili mashabiki wapate uhondo.

Onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts kwa hisani ya Dodoma Wine, Freditto Entertainment, CXC Africa na Saluti5. Mratibu huyo amesema kuwa siku hiyo Twanga Pepeta pia itapiga nyimbo zao za zamani zilizowapatia umaarufu. Baadhi ya nyimbo hizo ni Kisa Cha Mpemba, Fainali Uzeeni, Mtu Pesa, Safari 2005, Aminata, Busu  la mwaka2000, Nusu la kufunga mwaka na nyinginezo.

Bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino pia itapiga nyimbo zao kama Nyumbani ni Nyumbani, Dunia Daraja,‘Mwana Dar es Salaam’, ‘Shida ni Darasa’, ‘Rafiki Adui’, ‘Mwisho wa Ubaya ni Aibu’, ‘Nazi Haivunji Jiwe’, ‘Sitaki Tena’ na ‘Ganda la Miwa”. Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki kama Kalala Junior, Dogo Rama, Saleh Kupaza, Luiza Mbutu, Badi Bakule, Rama Pentagon, Frank Kabatano na Kalala Junior.
TWANGA PEPETA KUFANYA ONYESHO MAALUM LA VALENTINE DAY. TWANGA PEPETA KUFANYA ONYESHO MAALUM LA VALENTINE DAY. Reviewed by crispaseve on 04:29 Rating: 5

No comments

Post AD