Balozi Seif Atembelea hoteli ilioungua kwa moto Nungwi Kendwa.
Wahandisi wa Hoteli ya Kendwa wakijaribu kurejesha miundo mbinu ya umeme iliyoathirika kutokana na moto mkubwa uliotokea kwenye Hoteli hiyo.
Jengo la Jiko la Hoteli ya Kendwa Rocks lililoungua vibaya mwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mwakilishi
wa Hoteli ya Gold Zanzibar iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja
Bwana Andrea Azzala baada ya paa la jengo lao kuungua moto.
Balozi
Seif akikaguzwa kuangalia maeneo yaliathirikia kutokana na moto kwenye
Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kulia ya Balozi Seif ni Msaidizi
Menja Mkuu wa Kendwa Rocks Bwana Omar Ibrahim Kilupi, Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d.
Balozi Seif akiwafariji wamiliki wa
Kendwa Rocks Bwana Ali Ibrahim Kilupi aliyepo mwnzo kushto na msaidizi
wake Omar Ibrahim Kilupi baada ya jengo la jiko la hoteli yao kuungua
moto.Kati kati ni Waziuri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d
na kushoto kwa Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Kanal
Mstaafu Juma Kassin Tindwa.Picha na – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis OMPR
Hitilafu ya umeme
iliyotokea mapema asubuhi imesababisha moto mkubwa ulioteketeza jengo
la jiko, Duka ,sehemu ya burdani ya Hoteli Kendwa Rocks pamoja na
Hoteli ya Gold Zanzibar zilizopo katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa
kaskazini Unguja.
Moto huo ulioripuka
kwa kusaidiwa na upepo mkali uliokuwa ukivuma majira ya saa nne za
asubuhi umeteketeza vitu na vifaa mbali vilivyokuwemo ndani ya majengo
hayo na kusabisha hasara inayokisiwa kufikia shilingi za Kitanzania
Bilioni Moja { 1,000,000,000/- }.
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d
walifika eneo la tukio kuwafariji wamiliki wa Hoteli hizo.
Balozi Seif Atembelea hoteli ilioungua kwa moto Nungwi Kendwa.
Reviewed by crispaseve
on
05:56
Rating:
Post a Comment