NSSF yaanza rasmi usajili wa vijana Sports academy
Badhi ya wazazi wakiwasimamia watoto wao katika zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa
kushirikiana na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, limezindua mchakato wa usajili wa
vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga
na NSSF–Real Madrid Sports Academy.
Mchakato huo wa usajili umefanyika leo kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, ambako watoto kutoka Manispaa
za Ilala, Temeke na Kinondoni walisajiliwa na kuruhusiwa, zoezi linalotarajia
kuendelea leo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo,
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, aliwaka Watanzaia
kuwaleta vijana wao katika mchakato huo, na kwamba hakutakuwa na urasimu
utakaowakwamisha kusajiliwa.
Magori alisema kuwa, jukumu la kama NSSF ni kuratibu usajili
wa vijana wasiopungua 500, ambao watafanyiwa mchujo na Real Madrid kupata nyota
30 ambao wataingia rasmi katika darasa la kwanza kabisa la akademi hiyo
inayosubiriwa kwa hamu nchini.
“Wataalamu wanane wa lishe, tiba, afya na soka kutoka Madrid
watatua nchini wiki ijayo, kuwafanyia mchujo vijana wapatao 500 tunaotarajia
kuwasajili leo, kesho na wikiendi ijayo, ambao watafanya majaribio ya uwanjani
Februari 28,” alisema Magori.
Aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye vipaji,
kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwafikisha watoto wao kwenye usajili, ili
kuwawezesha kupata nafasi ya kuwania kuingia miongoni mwa wakali 30 wa awali
watakaofungua darasa la akademi hiyo.
Alibainisha kuwa, kutokana na uharaka wa uanzishwaji wa
kituo, NSSF na Real Madrid hawatoweza kutembelea mikoani kufanya usajili kama
huo mwaka huu, badala yake akawataka wazazi wanaoweza kufika na watoto wao Dar
es Salaam kufanya hivyo.
NSSF yaanza rasmi usajili wa vijana Sports academy
Reviewed by crispaseve
on
06:06
Rating:
Post a Comment