Header AD

MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KIDOGO KUTOKA ASILIMIA 4.0 MWEZI JANUARI, 2015 HADI KUFIKIA ASILIMIA 4.2 MWEZI FEBRUARI, 2015.

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei nchini kwa mwezi Februari, 2015. Kulia kwake ni Kaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa kazini wakati Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa ya kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei nchini kwa mwezi Februari, 2015. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
========  ======  =========
MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KIDOGO KUTOKA ASILIMIA 4.0 MWEZI JANUARI, 2015 HADI KUFIKIA ASILIMIA 4.2 MWEZI FEBRUARI, 2015.
 
Na: Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam,
09 Machi, 2015.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2015 umeongezeka  kwa asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.0  mwezi Januari mwaka 2015.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambapo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2015 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2015.

“Kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Februari, 2015 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Februari, 2015 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari, 2014, amesema Kwesigabo”.
MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KIDOGO KUTOKA ASILIMIA 4.0 MWEZI JANUARI, 2015 HADI KUFIKIA ASILIMIA 4.2 MWEZI FEBRUARI, 2015. MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KIDOGO KUTOKA ASILIMIA 4.0 MWEZI JANUARI, 2015 HADI KUFIKIA ASILIMIA 4.2 MWEZI FEBRUARI, 2015. Reviewed by crispaseve on 07:46 Rating: 5

No comments

Post AD