AUSTRALIA YAIPIGA ‘JEKI’ VETA
Mkurugenzi
wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi (kushoto) akitia saini ya makubaliano
kati ya Veta na Serikali ya Australia na Kulia ni Naibu Waziri Mkuu wa
Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hames
wanaoshudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi,Consolata Mgimba,Balozi wa Australia nchini,John Feakes katika
hafla ya makubaliano kati ya VETA na Serikali ya Australia iliyofanyika
leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba
akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati
ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika
Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi na akizungumza na waandishi habari
katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo
Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar
es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hames akizungumza
na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya
Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba
(Katikati),Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah
Moshi,kulia ni Naibu Makamu,Magharibi wa Australia,Waziri wa Afya na
Utalii,Dk.Kim Hames pamoja na watendaji wa VETA na Ubalozi wakiwa katika
picha ya pamoja katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt
Regency,jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MAMLAKA
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)imeanzisha mfumo wa mafunzo
stadi katika sekta ya madini na gesi ambao utasaidia watu wanaohitimu
katika mafunzo hayo duniani.
Hayo
ameyasema leo Mkurugenzi Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi wakati
wakisaini makubaliano na serikali ya Australia kuptia shirika la Idara
ya Mambo ya Nje na Biashara (DFAT)iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt
Regency,jijini Dar es Salaam.
Amesema
katika makubaliano hayo,Serikali ya Australia imekubali kutoa
Sh.milioni 330 kwa ajili mfumo huo ambao utatengenezwa na wataalam wa
nchi hiyo.
Mhandisi
Moshi amesema manufaa ya mfumo huo kwa VETA kuimarisha ushirikiano na
viwanda au waajiri mbalimbali, kulenga kutoa mafunzo ambayo yanaendana
na mahitaji ya soko la ajira,uboreshaji wa viwango vya mafunzo
yanayotolewa na viwanda,kuipunguzia mzigo serikali katika kuilea VETA
kwa kuchangia gharama za mafunzo kwa njia ya vifaa au kutoa wataalam wa
kufundisha.
Naibu
Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii
Dk.Kim Hemes amesema nchi yao imepiga hatua katika utoaji wa mafunzo
na viwango vyake vinatambulika duniani katika madini,mafuta,gesi pamoja
na Utalii.
AUSTRALIA YAIPIGA ‘JEKI’ VETA
Reviewed by crispaseve
on
09:54
Rating:
Post a Comment