Viongozi Waanzilishi TAPSEA Walalamikia Uchaguzi wa Chama Chao
Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko
madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na
katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari
mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.
Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko
madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na
katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari
mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.
MGOGORO
wa uongozi ndani ya Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA)
umeingia katika hatua tata baada ya viongozi waanzilishi wa chama hicho
kulalamikia uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 30, 2015 mjini Dodoma
ilhali kuna mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho ukiendelea.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya viongozi wenzake Mwenyekiti wa
TAPSEA, Pili Mpenda ambaye pia ni miongoni mwa waanzilishi wa chama
hicho jana jijini Dar es Salaam alisema anasikitishwa na kitendo cha
viongozi walioingia kinyume na katiba ya chama hicho kujipanga kufanya
uchaguzi ilhali kuna kesi ya msingi ipo mahakamani kulalamikia wao
kuondolewa madarakani.
Alisema
viongozi waliopo madarakani sasa wameingia kwa nguvu za Msajili wa
Vyama vya Siasa nchini baada ya kushinikiza uchaguzi kinyume na
maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza wa TAPSEA uliofanyika Arusha Mai 18,
2013 wa chama hicho ambao ulielekeza maboresho ya katiba ya chama kabla
ya chochote kufanyika.
Alisema
mkutano mkuu wa pili uliofanyika mkoani Mwanza 2014 uliitishwa ili
kuwaeleza wananchama juu ya shinikizo la msajili na wanachama wachache
(7) kufanyika uchaguzi na kuwaeleza mwenendo wa marekebisho ya katiba ya
TAPSEA lakini Ofisa msajili alishinikiza ufanyike uchaguzi ambao
uliwagawa wanachama na wengine kususia uchaguzi huo kutokana na
mvutano.
Bi.
Mpenda alisema uchaguzi uliofanyika haukuwa halali kwani mbali na
kufanyika kinyume na katiba ya TAPSEA na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa
kwanza haukushirikisha wanachama wote. Aliongeza kuwa kati ya wanachama
halali 815 waliokuwa wamejisajili ni wanachama 200 tu ndio walioshiriki
katika uchaguzi huo.
"...Uchaguzi
huu ni kinyume na katiba ya TAPSEA na kinyume na maelekezo ya Mkutano
Mkuu wa kwanza na ulifanyika kwa shinikizo la Msajili wa Vyama vya
Siasa...sisi hatujui alitumia kifungu gani kuja kushinikiza uchaguzi na
kuusimamia kinyume na katiba yetu," alisema Bi Mpenda katika mazungumzo.
Aidha
alisema tayari viongozi waliopinduliwa wameenda mahakamani kupinga
kitendo hicho na msajili anafahamu lakini wanashangaa kuona viongozi
wanaolalamikia wamejipanga kufanya uchaguzi mpya wa chama hicho Mai 30,
2015 mjini Dodoma. Hata hivyo taarifa kutoka kwa viongozi waliopo
madarakani kwa sasa wamekiri kujiandaa na uchaguzi mkuu mpya kwa nafasi
za juu za chama hicho pamoja na wajumbe 9 wa Kamati ya Utendaji.
Viongozi Waanzilishi TAPSEA Walalamikia Uchaguzi wa Chama Chao
Reviewed by crispaseve
on
00:54
Rating:
Post a Comment