BONDIA CHEKA KUPANDA ULINGONI MEI 30 P.T.A SABASABA JIJINI DAR KUZICHAPA NA MTHAILAND
BONDIA Fransic Cheka atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kabisa baada ya kutoka jela, ambapo atacheza na Kiatchai Singwancha kutoka
nchini Thailand ,mpambano huo wa raundi 10 utafanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam,
Akizungumza
matayarisho ya mpambano huo, promota Kaike Siraju amesema kuwa
amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda sawa kwa hivi sasa, ambapo
mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusainishwa wiki hii.
Mpambano huo utakaosimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini P.ST chini ya rais wake Emanuel Mlundwa
Wamesema kuwa wao wako tayari kwa
mpambano huo na bondia wa Thailand ataingia nchini siku tatu kabla ya
mpambano huo,ambao utavuta hisia za wapenzi wengi wa mchezo wa ndondi
nchini
Katika
mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo
wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali
kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi,pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
BONDIA CHEKA KUPANDA ULINGONI MEI 30 P.T.A SABASABA JIJINI DAR KUZICHAPA NA MTHAILAND
Reviewed by crispaseve
on
05:38
Rating:

Post a Comment