mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi yazinduliwa wilayani same.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela akizungumza na walimu (hawapo pichani) waliohuduria mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania na Mratibu wa
Basic Support Program Julius Lugemalila akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Elimu ya msingi TAMISEMI Kassim Kaoneka akiongea na
naibu Wazirir wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ,viongozi wa elimu na walimu
walioshiriki mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Same walioshiriki mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
Mwalimu Ruth Elifuraha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela amewataka
walimu wanaofanya kazi katika maeneo wanayotoka kuwa na nidhamu ya kazi
ili kuendelea kuinua ubora wa Elimu nchini.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya
walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same amesema sababu
kubwa ya kushuka kwa taaluma katika wilaya hiyo ni kutokana na walimu
kufundisha katika maeneo ya nyumbani. Kitu kinachosababisha muda mwingi kushughulikia matatizo ya familia zaidi.
"Walimu
wanaofundisha maeneo ya nyumbani mara nyingi hukosa nidhamu ya kazi kwa
kutofanya kazi uadilifu na badala yake kuishia kutatua matatizo
yanayozunguka ndugu na jamaa" alisema Naibu Waziri.Aidha, amewataka kuwa
na nidhamu ya hali ya juu ili kuhakikisha wanawatendea haki watoto
wanaowafundisha na kuheshimu muda wa serikali kwa kufanya kazi kwa masaa
wanayopaswa kufanya kazi.
Serikali
ilianzisha Programu ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi ili
kukabiliana na changamoto za kushuka kwa kiwango cha ufaulu. Programu
hii iitwayo Programu ya Mafunzo ya Kujenga Uwezo kwa Walimu na Wanafunzi
katika ujifunzaji na ufundishaji inalenga kuongeza kiwango cha ufaulu.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi ngazi ya shule yanasimamiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Srikali za Mitaa (TAMISEMI).
Ufuatiliaji wa mafunzo unafanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi.
mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi yazinduliwa wilayani same.
Reviewed by crispaseve
on
11:58
Rating:
Post a Comment