Header AD

SOMA ALICHOZUNGUMZA MH. MWIGULU WAKATI AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS JIONI YA LEO



#‎YALIYOJIRI‬ MTU ANASTAAFU HALAFU UNAMUONGEZEA MUDA WA NINI WAKATI KUNA VIJANA HAWANA AJIRA - MWIGULU
SOMA ALICHOZUNGUMZA MH. MWIGULU WAKATI AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS JIONI YA LEO
Mwigulu: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwaajili ya nchi yetu
Mwigulu: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama
Mwigulu: Nilipomaliza shahada ya 2 nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana
Mwigulu: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili
Mwigulu: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea
Mwigulu: Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo?
Mwigulu: Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya.
Mwigulu:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua
Mwigulu: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Mwigulu: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana
Mwigulu: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo
Mwigulu: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa.
Mwigulu: Mtu anabakiza muda mchache hadi anakuja kustaafu unamuongezea muda tena kazini wakati kuna vijana wasio na kazi
Mwigulu: Ninaposema kukomesha rushwa nitazingatia maslahi ya Wafanyakazi, haiwezekani wengine Wale kidogo na wengine kubwa
Mwigulu: Mtu anayeiba dawa ambazo zingemtibu maskini huyo ni mhujumu, tutamnyang'anya leseni yake na atakwenda jela.
Mwigulu: Tutasimamia Muungano wetu maana sio wa vitu ila ni watu. tutahakikisha uchumi wa Zanzibar nao utapewa kipaumbele
Mwigulu: Nawaambieni nawaomba kazi hii nikiwa bado nina nguvu ili niweze kufika mwenyewe maeneo yenye migogoro ya ardhi.
Mwigulu: Ninapotangaza nia ya jambo hili nimetathimini vya kutosha na nikajiridhisha na ahadi yangu ni kwamba nitawavusha.
Mwigulu: Tunaposimamia kuacha kufanya kazi kwa mazoea ndio tunasema mabadiliko ni vitendo na wakati ni sasa
Mwigulu: Ukiwaondoa vijana mjini wakati wakifanya kazi halali kwa kigezo cha uchafu,watarudi mjini na kufanya kazi haramu
Mwigulu: Natangaza rasmi kuomba ridhaa ya kugombea katika chama changu ili niweze kuleta mabadiliko Katika Nchi yangu.
Mwigulu: Napoenda kupigana vita hii siendi kupigana kwaajili ya Watanzania ila mimi mwenyewe maana umaskini unanigusa.
Mwigulu: Mambo matatu ninayowaomba Watanzania ni kwamba mniamini, pili mniunge mkono na tatu nitawavusha.
SOMA ALICHOZUNGUMZA MH. MWIGULU WAKATI AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS JIONI YA LEO SOMA ALICHOZUNGUMZA MH. MWIGULU WAKATI AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS JIONI YA LEO Reviewed by crispaseve on 10:26 Rating: 5

No comments

Post AD