Header AD

TASNIA YA SANAA NA UTAMADUNI KUTUMIKA KUENDELEZA AMANI NA UPENDO NCHINI.

0029Na: GenofevaMatemu – Maelezo
……………………………………………….
Wadau waTasniaya Sanaa na Utamaduni wametakiwa kutumia Sanaa kuendeleza upendo, amani na uvumilivu wa nchi hasa katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi makuu.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Helmas Mwansoko alipokua akimwakilisha Mhe.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni kwenye maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Prof. Mwansoko amesema kuwa suala la upendo linasisitizwa katika vitabu mbalimbali vya dini ulimwenguni kote kwani palipo na upendo amani na utulivu vinatawala hivyo kuwaomba wadau wa Sanaa na utamaduni kutumia mbinu mbalimbali za sanaa kuendeleza upendo na amani nchini.
“Nikinukuu kwenye katiba inayopendekezwa sura ya kwanza Ibara ya tano inasema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa ambapo moja ya tunu hizo ni Amani nautulivu pia sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 kipengele cha dhima ya utamaduni kimeeleza kuwa watanzani awanajivunia kuwa kielelezo cha Uhuru na utaifa wao kwakuwa na umoja, amani na utulivu hivyo ni vyema tukaendeleza amani ya nchi yetu kupitia sanaa”, alisema Prof. Mwansoko.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bibi Jacqueline Maleko amesema kuwa TanTrade imeandaa mpango mkakati wa kukuza na kuendeleza biashara ya bidhaa za asili za Tanzania kuweza kupata masoko ndani na nje ya nchi hivyo kuchangia katika kukuza kipato kwa wadau na uchumi waTaifaletu.
Bibi. Maleko amesema kuwa vitu vya asili kutoka Tanzania vinapendwa na watu kutoka nchi nyingine hivyo kuwataka wadau wa Tasnia ya Sanaa na Utamaduni kuchangamkia fursa zinazo jitokeza na kupigania kupata masoko endelevu ya bidhaa nakujitokeza kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya Sanaa na utamaduni yatakayo wawezesha kupata mbinu mpya za kiujasiriamali.
Siku ya uanuaiwa utamaduni uadhimishwa duniani kote kila tarehe 21 ya mwezi wa tano ambapo nchini Tanzania siku hiyo imeadhimishwa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba na kubeba kaulimbiu iliyosema “Tuuenzi Utamaduni wetu kwakudumisha Amani na Upendo wakati wa Uchaguzi Mkuu” na kushirikisha wajasiriamali mbalimbali wabidhaa za utamaduni pamoja wasanii kutoka Kituo cha Utamaduni cha India kilichopo nchini Tanzania.
TASNIA YA SANAA NA UTAMADUNI KUTUMIKA KUENDELEZA AMANI NA UPENDO NCHINI. TASNIA YA SANAA NA UTAMADUNI KUTUMIKA KUENDELEZA AMANI NA UPENDO NCHINI. Reviewed by crispaseve on 01:09 Rating: 5

No comments

Post AD