MITAZAMO HASI KITAMADUNI CHANZO CHA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues,
akiwasilisha mada katika warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji
cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kuhusu ushirikishaji
jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na
kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye
albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi
wa dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).(Picha zote na
Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewjiblog team, Mwanza
Mauaji
ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) yanayoendelea nchini
yanatokana na mitazamo hasi kitamaduni miongoni mwa wanajamii. Hayo
yameelezwa na washiriki wa warsha ya siku tatu inayoendelea katika
kijiji cha Nyakahungwa kata ya Nyakahungwa wilayani Sengerema yenye
lengo la kubadili mitazamo iliyojengeka katika jamii na kusababisha
madhara makubwa kwa watu wenye albinism iliyoandaliwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Warsha
hiyo ni miongoni mwa mlolongo wa warsha nne zitakazofanyika katika
wilaya za Sengerema, Mwanza, Kahama na Bariadi kwa kuzishirikisha jamii
kuibua masuala mbalimbali yanayobagua, kunyanyapaa na kuwatenga watu
wenye albinism katika maeneo husika. Warsha hizo
zinafanyika katika kipindi ambacho kumetokea mauaji ya mtoto wa kike,
msichana na kijana wenye albinism wilayani Sengerema wakati tarehe 14
Mei 2015 mwanamke mmoja alikatwa mkono wilayani Bariadi.
Afisa
Maendeleo ya Jamii wilaya ya Sengerema, Bw. Bushaija Vicent (kulia),
akitoa takwimu za idadi ya za wanafunzi wenye albinism katika wilaya
yake kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira Rodgrigues.
Kwa
mujibu wa Afisa Maendeleo Jamii wilayani Sengerema Bwana Bushaija
Vicent kati ya shule za msingi 191 wilayani humo ni Shule zenye watoto
wenye albinism ni 14, Idadi yao ni 16 katika shule ya awali watoto 4
wana albinisim, vyuo mbalimbali Sengerema vijana 4 wana albinism na
katika Shule za sekondari 48, watoto wenye albinism 4.
MITAZAMO HASI KITAMADUNI CHANZO CHA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM
Reviewed by crispaseve
on
01:16
Rating:
Post a Comment