Header AD

UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI

Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya matumizi ya Tehama katika ufundishaji kwenye vyuo vya ualimu.Na Geofrey Adroph, Pamoja blog
Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu ya Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limejikita katika uboreshaji wa elimu kwa kuwapa mafunzo walimu katika somo la Teknnolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama). 

  Akizungumza leo katika Ufungaji wa Mafunzo yaliyoandaliwa na UNESCO wakishirikiana na China Funds in Trust Project (CFIT) yaliyofanyika kwa siku tano katika Ukumbi wa DIT, Jijini Dar es Salaam, Ofisa Miradi wa UNESCO, Faith Shayo amesema mafunzo waliopata walimu wa vyuo vya walimu mbalimbali nchini itawasaidia katika uboresha wa elimu ikiwa ni pamoja na kuwapa vifaa vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo.
UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI Reviewed by crispaseve on 06:40 Rating: 5

No comments

Post AD