Bayport yazindua huduma mpya ya mikopo ya viwanja kwa Watanzania wote
Mkurugenzi
wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani, akizungumza jambo
katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja katika mradi wa
Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa ya Mei
22, katika Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo
viongozi wa serikali. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida, taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services,
inayojihusisha na mikopo, imeanzisha huduma mpya ya kukopesha viwanja watumishi
wa umma, wafanyakazi wa kampuni za kawaida na wajasiriamali wa aina zote.
Kuanzishwa
kwa huduma hiyo mpya kumetokana na taasisi hiyo kupania kuboresha maisha ya
Watanzania, likiwamo kundi la wajasiriamali ambalo limeendelea kusahauliwa na
kampuni nyingi kupewa mikopo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, akizungumza katika uzinduzi huo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mwishoni
mwa wiki katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mtendaji wa
Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema kuwa ni kusudio lao kutoa fursa ya watumishi
wa umma, wafanyakazi wa kampuni na wajasiriamali kupata nafasi ya kutimiza
ndoto za kumiliki ardhi nchini Tanzania.
Mwakilishi
wa Mkuu wa wilaya Kibaha, Obed Katonga, kulia akijadiliana jambo na
Meneja Uzalishaji wa Bayport Financial Services, Mashaka Mgeta kulia
kwake na Mkuu wa Kanda ya Pwani, David Ndiega.
“Huduma
yetu
katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani, fomu zake zinapatikana
katika
matawi yote ya Tanzania Bara, ambapo kwenye matawi yetu yote fomu hizo
zitakuwapo, huku fomu hizo za kukopeshwa viwanja zikipatikana kwa wiki
mbili, kuanzia Mei 22 hadi Juni 10 mwaka huu.
“Si lazima
uwe mtumishi wa umma ili uwe na sifa ya kukopeshwa viwanja, ila hata
wajasiriamali nao wamekumbukwa katika huduma hii nzuri kwa Watanzania wote,
hivyo ni wakati wao sasa kuiunga mkono taasisi hii ili iweze kuwakomboa na
kuwakwamua pia,’ alisema Mbaga.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda mwenye shati jeupe mbele akiwa
katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja kutoka kwenye
taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana jijini Dar es
Salaam. Mwenye miwani ni Ruth Bura, mtumishi wa taasisi hiyo anayehusika
na mambo ya Bima.
Akimwakilisha
Mkuu wa wilaya ya Kibaha katika uzinduzi huo, Afisa Mipango wa wilaya hiyo,
Obed Katonge, alisema kwamba Bayport imebuni huduma nzuri inayofaa kuungwa
mkono na Watanzania wote, hasa kwa kuingia kwenye sekta ya ardhi inayopanda
thamani siku hadi siku duniani kote.
Wadau wanafuatilia uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akiendelea
kufafanua katika uzinduzi wa mikopo ya viwanja, katika Hoteli ya Serena,
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kushoto
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa
serikali.
Meneja
Masoko wa Property International, Zora Moore, akizungumza katika
uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, huku wao wakiwa ni kampuni
iliyohusika na upimaji wa viwanja hivyo vya Vikuruti, Wilayani Kibaha,
mkoani Pwani.
Mambo
yamekwenda poa. Ndivyo wanavyoonekana kusema Mkurugenzi Mtendaji wa
Bayport Financial Services, John Mbaga kulia na Meneja Masoko wake na
Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, katika uzinduzi wa mikopo ya
viwanja. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es
Salaam.
Mwandishi
wa Clouds Tv na Radio, Salehe Masoud, akibadilishana mawazo na mdau wa
maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, mwenye shati
jeupe na Mwandishi wa redio ya Times FM, Phillip Daudi.
Staff wa Bayport Financial Services wakijadiliana katika uzinduzi wa huduma yao.
Wadau wanafuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea katika uzinduzi huo.
Baada ya kuzindua, wadau walikuwa wakibadilishana mawazo kama hivi.
Bayport yazindua huduma mpya ya mikopo ya viwanja kwa Watanzania wote
Reviewed by crispaseve
on
06:38
Rating:
Post a Comment