BENKI YA NMB YAZINDUA RASMI FAMILIA YA KADI ZA BENKI “MASTERCARD DEBIT” ZINAZOKUBALIKA KIMATAIFA
Wadau
wa benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza kwa umakini
hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu
Mhe. Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
MasterCard itakayoanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Uzinduzi huo
ulifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback,
akiwahutubia wadau wa Benki ya NMB wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi
hiyo mpya ambayo itaanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Hafla hiyo
ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti
wa bodi, benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja (kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) wakati wa
uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard iliyozinduliwa rasmi na benki
hiyo katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. (Kulia) ni
Afisa wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback
aliyehudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti
wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja (kushoto), Mkurugenzi mkuu
wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (katikati) pamoja na Rais wa Master
Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback, (kulia) wakiteta
jambo kabla ya uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza
kutumika katika benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Hyatt
Regency jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akimkaribisha Rais mstaafu
wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika
hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa
rasmi na wateja wa benki hiyo hivi karibuni. (Anayeangalia kulia) ni
Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Prof. Joseph Semboja. Hafla hiyo
ilifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam.
Rais
mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa (kushoto)
akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya NMB, Prof. Joseph Semboja mara
baada ya kuwasili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam
rasmi kwa kuzindua huduma mpya ya Mastercard iliyoanzishwa na benki
hiyo.(Katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker.
Rais
mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin W. Mkapa (kushoto) akisalimiana
na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback
(kulia) mara tu alipowasili katika uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard
itayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo. (Katikati) ni
Mkurugenzi mkuu wa benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker.
Rais
wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback akifafanua
jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard
itakayoanza kutumiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli
ya Haytt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti
wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa wadau
wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza
kutumika hivi karibuni kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika
hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam.
Rais
mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa akihutubia wadau wa
benki ya NMB kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Mastercard ya benki
ya NMB ambayo itatumika rasmi kwa wateja wake hivi karibuni. Hafla
iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro Hotel.
Mwenyekiti
wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari mara tu baada Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe.
Benjamin W. Mkapa kuzindua rasmi huduma mpya ya NMB Mastercard. Hafla
hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency, jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa
(katikati) pamoja wakurugenzi wa Benki ya NMB wakikishangilia kikundi
cha sanaa kilichotumbuiza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
MasterCard itakayoanza kutumika kwa mara ya kwanza kwa wateja wake.
Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro,
jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam, Tanzania, 16 June 2015 –National Microfinance Bank (NMB),
Benki inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi nchini, imezindua rasmi
familia ya kadi za benki “MasterCard Debit”, zikiwemo Tanzanite,
Titanium kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Kadi ya “First world Rewards”.
Familia
hii ya kadi hizi za benki zitahudumia wateja aina mbalimbali, ikiwemo
asilimia kubwa ya wateja (Tanzanite), wateja wa kipato cha kati
(Titanium) na wale wateja wa kipato cha juu (World Rewards) ikitoa
huduma na faida mbalimbali mahususi kwa walengwa.
“Pamoja
na ukuaji wa kasi katika sekta ya malipo kwa njia ya elektroniki,
wateja wetu wanazaidi kutafuta njia za haraka, salama na zenye unafuu
kutumia katika malipo. Kukabiliana na wimbi hili, tumezindua familia hii
ya kadi zinazokubalika kimataifa, na hivyo kurahisisha upatikanaji wa
pesa zao kwa usalama popote walipo, Tanzania au nje ya nchi” alisema
Ineke Bussemaker, Mkurugenzi mtendaji wa NMB.
Wamiliki
wa kadi hizi za ‘MasterCard’ wataweza kutoa Fedha kutoka mashine za
Miamala ya fedha duniani kote zenye alama ya “MasterCard Acceptance” ya
fedha. Pia wataweza kulipia bili, kulipia umeme na Salio za simu, pamoja
na kununua bidhaa mtandaoni kutoka maduka mbalimbali makubwa ndani na
je ya nchi.
“Kadi
za “MasterCard debit” zinakubalika na mamilioni ya wafanya biashara
kutoka nchi Zaidi ya 210, ikiwa na maana kuwa wanaosafiri kwa ajili ya
mapumziko au biashara wataweza kupata pesa zao popote pale, kwa urahisi
kama wakiwa nyumbani” alisema Michael Miebach, Raisi, Mashariki ya kati
na Africa, MasterCard.
“muhimu
Zaidi, kila muamala wa kitaifa na kimataifa unalindwa na usalama wa
“masterCard SecureCode pamoja na EMV chip na Teknolojia ya PIN” ambazo
hutoa usalama wa ziadakila mara mteja anatumia kadi yake mtandaoni au
katika duka la kawaidia.”
NMB
pia inakuwa Benki ya kwanza Tanzania kuzindua kadi ya “MasterCard World
Rewards”. Kadi hii inawapa fursa wamiliki kupata huduma za kipekee za
kiamisha kama vilie ofa za ndege, malazi, kukodisha gari, vyakula,
manunuzi, michezo na burudani kupitia “Mastercard priceless Cities and
Priceless Africa Programmes”.
“Hapa
NMB tunaamini ni muhimu kufahamu mahitaji na matakwa ya wateja wetu, na
kuwazawadia kutokana uaminifu wao. Tunayofuraha kuwa benki ya kwanza
Tanzania kutambulisha mpango huu wakimapinduzi unaotoa zawadi kwa wateja
wetu wa kipato cha juu huduma mbalimbali za kipekee za kimaisha,
kupitia matawi yetu yaliyopo tayari na tawi letu jipya kabisa la
“Private banking” litakalo hudumia wateja wetu wa kipato cha juu”
alisema Bussemaker.
Wamiliki
wa kadi za “Worlds Rewards” wataweza kujipatia poinyti za uaminifu kila
mara wanapotumia kadi zao. Pointi hizi za uaminifu zinaweza kukombolewa
kwenye mashirika ya ndege zaidi ya 800 dunia nzima, kampuni za
kukodisha magari an hoteli maarufu Zaidi ya 160,000 duniani.
Wamiliki
wa kadi zilizo kwenye familia hii, wataenedlea kufurahia huduma
nyinginezo za NMB zikiwemo “NMB App, NMB Internet Banking, NMB
E-Statement na NMB Mobile”.
Kuhusu NMB
National Microfinance Bank (NMB) ndio benki ya biashara inayoongoza
kwa huduma zote kamilifu hapa Tanzania ikitoa huduma mbalimbali za
kibenki kwa kundi la wateja linalowakilisha vyema Tanzania nzima. Benki
hii hutoa huduma kama za akiba, mialama pamoja na huduma za ufadili kwa
watu binafsi, kuanzi kampuni ndogo hadi za kati, serikali, kilimo
biashara pamoja na makampuni makubwa na taasisi. NMB pia ina jukumu
muhimu katika sekta ya kilimo pamoja na maghala hapa nchini kupitia
SACCOS na Amcos.
Katiaka
Ubinafsishaji mwaka 2005, benki ilikuwa na wateja takribani 600,000,
idadi hiyo ikiongezeka na kufikia millioni 1.8. Benki haikuwa na Mashine
ya muamala (ATM) hata moja miaka mitano iliyopita, leo hii inamiamala
Zaidi ya 600, ambayo ni asilimia 40 ya mashine zote Tanzania kwa ujumla.
Benki inamatawi zaidi ya 170 na inapatikana katika asilimia 95 ya
wilaya zote za kiserikali Tanzania. Nia ya benki hii ni kufikia asilimia
100 ya wilaya zote Tanzania
Fuatilia ukurasa wetu Twitter @NMBTanzania na upande wa Facebook NMB Tanzania
Kuhusu MasterCard
MasterCard, www.mastercard.com, ni
kampuni ya teknolojia katika ulimwengu wa malipo ya kielektroniki. Sisi
tunaendesha mfumo wenye kasi zaidi duniani katiaka masuala ya miamala
ya fedha, kuunganisha wateja, taasisi za fedha, wafanyabiashara,
serikali na biashara katiaka nchi zisizopungua 210. Bidhaa hizi za
MasterCard pamoja na huduma zake hufanya shughuli za kibiashara za kila
siku kama vile ununuzi, kusafiri, kuendesha biashara na kusimamia fedha -
rahisi, salama zaidi na zenye ufanisi zaidi kwa kila mtu. Fuatilia
kurasa wetu wa Twitter: @MasterCardMEA na @MasterCardNews, kujiunga na majadiliano Beyond the Transaction Blog na jiunge kupata habari za kina MEA Engagement Bureaua.
BENKI YA NMB YAZINDUA RASMI FAMILIA YA KADI ZA BENKI “MASTERCARD DEBIT” ZINAZOKUBALIKA KIMATAIFA
Reviewed by crispaseve
on
07:13
Rating:
Post a Comment