POLISI ALIYENASWA AKIMNYANYASA BINTI MWEUSI TEXAS AJIUZULU
Ofisa huyo wa polisi akimhenyesha binti wa miaka 15.
Eric Casebolt (41) akiwa amembana binti huyo.
Video ya tukio hilo iliyowekwa Jumamosi Youtube ikiwa imetazwa na zaidi ya watu milioni 10.
OFISA wa Polisi katika Jimbo la Texas, Marekani, Eric Casebolt (41)
aliyenaswa kwenye video akimnyanyasa binti mweusi kwa kumkamata na
kumdondosha chini kisha kutoa bastola akiwalenga vijana wengine wawili
amejiuzulu. Taarifa zimeeleza kuwa ofisa huyo ameamua kujiuzulu kwa
utashi wake mwenyewe jana Jumanne.
Ofisa huyo akiwalenga vijana wawili kwa bastola.
Tukio hilo lililonaswa eneo la McKinney Ijumaa iliyopita
linamuonyesha ofisa huyo ambaye ni mzungu akimfunga pingu binti wa miaka
15 baada ya kumdondosha chini bila huruma kisha kuwalenga na bastola
yake vijana wengine wawili waliokuwa katika pati eneo hilo. Baada ya
tukio hilo, ofisa huyo alisimamishwa kazi.
Waandamanaji wakipinga tukio hilo.
Polisi huyo na wenzake walifika eneo hilo baada ya kuitwa na wenyeji
waliokuwa wanalalamikia kuwepo kwa vurugu katika sherehe hizo zilizokuwa
zinafanyika kwenye bwawa la kuogelea.Baada ya tukio hilo kuenea mitandaoni, mamia ya waandamanaji waliandamana kuelekea eneo hilo wakitaka ofisa huyo afukuzwe kazi.
POLISI ALIYENASWA AKIMNYANYASA BINTI MWEUSI TEXAS AJIUZULU
Reviewed by crispaseve
on
22:21
Rating:
Post a Comment