SIMBACHAWENE ATAKA USHIRIKIANO ATEKELEZE MAJUKUMU YA WIZARA
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwilowe, Wilaya ya Mpwapwa, baada kuzuia msafara wake wakati alipopita katika
Kijiji hicho wakati wa ziara ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme
Vijijini Awamu ya Pili unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
na Kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO). Wanakijiji hao
walimweleza Waziri kuwa kijiji chao pia kiunganishwe na umeme.
Wananchi
wa Kijiji cha Mwilowe wakizuia msafara wa Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene wakitaka kijiji hicho pia kiunganishwe na nishati
hiyo. Waziri alikua katika ziara ya kutembelea na kukagua Utekelezaji wa
Mradi wa Umeme Vijijini unaofadhiliwa na wakala wa Nishati Vijijini
(REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiangalia mfano wa mashine ya kusaga inayotumia umeme wa
mota aliyotengenezwa na Kijana katika Kijiji cha Lukole. Simbachawene
aliahidi kumsaidia Kijana hiyo kuweza kufikia lengo lake.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizindua Albam ya nyimbo ya Kwaya ya Mtakatifu Agustino katika Kijiji cha Kingiti,
Kigango cha Kingiti, wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kukagua
Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene akionesha Album ya nyimbo ya
Kwaya ya Mtakatifu Agustino katika Kigango cha Kingiti, kijiji cha
Kingiti baada ya kuzindua Albam hiyo. Simbachawene alizindua album hiyo
wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini,
Awamu ya Pili.
Waziri
wa Nishati na Madini, George simbachawene akishiriki kucheza ngoma ya
Kabila la Wagogo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Umeme
Vijijini, Awamu ya Pili katika Kijiji cha Malolo, Wilaya ya Mpwapwa,
Mkoani Dodoma.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene akimkabidhi baskeli , Diana
Kalenza, katika kijiji cha Idodoma, Wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara
yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme vijijini, Awamu ya Pili. Kwa mujibu wa Simbachawene baiskeli hiyo imetengenezwa na SIDO, Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi katika kijiji cha Malolo akiimba wimbo mbele
ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa ziara ya
Waziri katika Kijiji chicho. Wimbo huo uliokuwa na ujumbe wa kumwomba
waziri kukiunganisha Kijiji hicho. Aidha, wimbo huo ulieleza namna wanakijiji hao watakavyotumia nishati hiyo kwa maendeleo yao.
Na Asteria Muhozya, Mpwapwa
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewataka wananchi kuwapa
ushirikiano viongozi wa Wizara hiyo ili waweze kutekeleza kikamilifu
majukumu yao kutokana na kusimamia rasilimali muhimu zinazobeba uchumi
wa nchi.
Simbachawene
aliyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake ya kukagua
utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unafadhiliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO),
katika vijiji vya Kinusi, Nzugilo, Idodoma, Malolo na Lukole, Wilaya ya
Mpwapwa, Mkoani Dodoma.
“Tuko
kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Tunataka mshuhudie mafanikio makubwa
ya usambazaji umeme vijijini. Serikali inatambua umuhimu wa nishati hii
kwa maendeleo,na tutahakikisha kuwa, tunavifikia vijiji zaidi katika
Awamu ya Tatu”, alieleza Simbachawene.
Simbachawene
aliongeza kuwa, Mradi wa usambazaji Umeme Vijijini ni endelevu na
kuongeza kuwa, hivi sasa , serikali imezifikia takriban Kata na
Tarafa nyingi nchini na kuongeza kuwa, serikali itahakikisha inayafikia
maeneo mengi zaidi yakiwemo yale yenye huduma muhimu za kijamii
zikiwemo zahanati, shule na visima vya maji.
Aidha,
alisema wizara yake iko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote
kuhakikisha kwamba wananufaika na rasilimali anazozisimamia bila kujali
itikadi za vyama na hivyo kuwaomba wananchi kuonesha ushirikiano wakati
serikali inapotekeleza Mradi huo wa usambazaji umeme Vijijini.
“Tuo
kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si kwa kuangalia itikadi za
vyama.Tutawatumikia wananchi wote bila kupokea rushwa kwa kuwa tunao
uwezo wa kuwatumikia , nia tunayo, tunachotaka ni ushirikiano wenu”,
alisema Simbachawene.
Katika
hatua nyingine Simbachawene amepiga marufuku uchimbaji wa madini katika
vyanzo vya maji na kueleza kuwa, wote watakaobainika kuchimba madini
katika vyanzo hivyo, watafutiwa leseni zao za uchimbaji madini.
“
Sheria ya madini, kanuni na taratibu zake haziruhusu kuchimba madini
katika vyanzo vya maji, kwa yeyote atakaebainika kuchimba madini katika
vyanzo hivyo, tutamfutia leseni kwa kufuata taratibu na kanuni
hizo”,alisistiza Simbachawene.
SIMBACHAWENE ATAKA USHIRIKIANO ATEKELEZE MAJUKUMU YA WIZARA
Reviewed by crispaseve
on
09:35
Rating:
Post a Comment