TIMU YA VITO FC YAAGWA NA KUAHIDI KUREJEA NA USHINDI
Balozi
wa Finland nchini Tanzania Bibi. Sinikka Antila akifurahia jambo na
wachezaji wa Timu ya VITO FC kutoka Kilwa mkoani Lindi, ambayo ilikuwa
inaagwa jana kwaa ajili ya kuelekea nchini Finland kwa ajili ya
kushiriki michuano ya Kombe la Helsinki itakayoanza kutimua vumbi tarehe
05 Julai jijini Helsinki Finland. Timu hiyo imepata ushiriki huo
kupitia Asasi ya kirai ya Sports Development Aid (SDA) ikiwa na lengo la
kutumia michezo kama nyenzo ya kuhamasisha jamii kuwapeleka watoto wao
wakapate elimu.
Meneja
Mradi wa Sports Development Aid (SDA) Bw. Mohamed Chigogolo akielezea
jambo wakati wa hafla ya kuwaaga watoto wanaoenda kushiriki michuano ya
Kombe la Helsinki nchini Finland, hafla hiyo imefanyika jana katika
ukumbi wa Ubalozi wa Finland jijini Dar es Salaam.Katikati ni Afisa
Michezo Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo Bw.
Nicholaus Bulamile na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface
Wambura akipeana mkono wa mmoja wa wachezaji wa timu ya Vito FC ya
wilayani Kilwamkoa wa Lindi wakati wakiagwa kwa ajili ya kuelekea nchini
Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo
kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya
timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo
yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu
1000.
Balozi
wa Finland nchini Bibi. Sinikka Antila akipeana mkono wa mmoja wa
wachezaji wa timu ya Vito FC ya wilayani Kilwamkoa wa Lindi wakati
wakiagwa kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la
Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini
ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na
kushirikisha zaidi ya timu 1000.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface
Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Vito FC ya
Kilwa mkoani Lindi wakati wa hafla ya kuwaga kwa ajili ya kuelekea
nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini
humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla
ya timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo
yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu
1000.Picha na Frank Shija, WHVUM.
TIMU YA VITO FC YAAGWA NA KUAHIDI KUREJEA NA USHINDI
Reviewed by crispaseve
on
00:33
Rating:
Post a Comment