KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAGAWA ZAWADI ZA EIDD EL FITR KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada
wa vitu mbalimbali kwa mtoto Sophia Said wa kituo cha Yatima cha Maunga
cha Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni masandalizi ya Sikukuu ya
Idd El Fitr.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwakabidhi sehemu ya
msaada wa vitu mbalimbali watoto, Gatson Edward na Bonny Mayanga wa
kituo cha Yatima cha Tuwakomboe cha Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni
masandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitir. Jumla ya vituo 10 vilinufaika
na msaadahuo ambao umetokana na mapato ya Tamasha la Pasaka la mwaka
huu.
Sehemu ya misaada hiyo ikishushwa
KAMPUNI
ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, jana iligawa
misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi mil 9.5 kwa vituo 10 vya kulea yatima vya jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi
misaada hiyo kwa viongozi na wawakilishi wa vituo hivyo, Msama mwasisi
wa matamasha ya Injili nchini tangu mwaka 2000, alisema ametoa vitu
hivyo kuwapa faraja watoto wa vituo hivyo.
Msama ambaye hivi karibuni alitoa msaada kama huo
wenye thamani ya shilingi mil 7.5, alisema msaada huo wa jana ni kuwapa
faraja watoto hao kufurahia sikukuu ya Idd el Fitr inayoweza kuangukia
kati ya Julai 18 au 19.
“Nimeguswa
kuendelea kusaidia watoto hawa, najisikia faraja na amani ya moyo
ninapofanya hivi nikikumbuka mbali mno, ikiwemo hata maisha niliyowahi
kuishi na kuyapitia, hivyo si kutaka sifa wala umaarufu,” alisema.
Msama
ametoa wito kwa jamii kutambua watoto wanaolelewa katika vituo hivyo si
kupenda kwao, bali ni kutokana na changamoto za kimaisha zilizowapata
hadi ku kila mtoto angependa kulelewa na wazazi wake.
Vituo vilivyopewa msaada wa vitu mbalimbali kama unga, mchele, sukari, sabuni na juisi, ni Honoratha, Mwana, Umra, Mujahidina, Zaidi, Hairat, Sifa, Mwandaliwa na Chakuwama.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo, Alhaji Mzee ambaye ni mmoja wa watoto wa
kituo cha Alhaji Mzee wa kituo cha Mwandaliwa, alisema ni furaha kubwa
kwao kupata msaada huo kuelekea sikukuu hiyo.
Msama
alisema fedha zilizotumika kununua vitu hivyo ni kutoka katika mfuko wa
Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2000 chini ya
uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.
Msama
ni mtu aliyejipambanua kama mdau mkubwa katika kusaidia jamii kupitia
makundi maalumu kama yatima, walemavu na wajane kwa lengo la kuwapa
faraja ya kufurahia maisha kama wengine.
Mbali
ya kutoa misaada mbalimbali kwa makundi hayo kabla au baada ya tamasha
la Pasaka kila mwaka, Msama amewahi kusaidia waathirika wa mabomu ya
Gongo la Mboto, mwaka 2011
KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAGAWA ZAWADI ZA EIDD EL FITR KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR
Reviewed by crispaseve
on
02:28
Rating:
Post a Comment