SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO PIA YAZINDUA TOVUTI.
Afisa
Mtendaji Mkuu EAG Group Iman Kajula Wa Pili (kushoto) akipokea hati ya
Kimila ya eneo walillonunua bagamoyo kwajili ya Jumuiya hiyo.
Jumuiya
iliyoasisiwa na wakazi wa Kilima hewa Salasala jijini Dar es salaam
likiwa na malengo ya kijamii na kiuchumi. Tangu kuasisisiwa SVG
imetekeleza miradi Mingi kwenye eneo la Salasala ikiwemo kupanda miti
zaidi ya 5,000, kutengeneza barabara, kutengeneza viwanja vya michezo
na kulinda maeneo ya wazi, Ulinzi, kutengeneza gari la polisi na
misaada ya miradi mbalimbali endelevu ikiwamo kujenga ofisi ya Serikali
ya Mtaa Salasala
SVG
haikuishia hapo, imeamua kwa dhati kuchochea maendeleo ya Wanachama
wake. Mradi mkubwa uliotekelezwa ni pamoja na kununua hekari 250 huko
Fukayosi Bagamoyo. Baada ya ununuzi huu mchakato wakupata hati ulifanywa
na kufanikiwa kupata hati za kimila na kukabidhiwa kwa wanachama wa SVG
ili kuanza kuendeleza maeneno hayo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Afisa Aridhi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Kibona
aliipongeza SVG kwa kuwa kikundi kilicho makini na kutumia dhima ya
umoja ni nguvu, alisema hati za kimila zina faida nyingi sana ikiwamo
kutokuwa na kipindi cha ukomo ikilinganishwa na hati za
kawaida.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa SVG Yahaya Banka alisema ‘’ SVG inalenga
kuendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wanachama wake na familia zao.
Tunaamini kwa kutumia nguvu ya umoja tunaweza kuleta maendeleo makubwa
katika eneo letu tunaloishi pia kwa familia za wanachama’’
SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO PIA YAZINDUA TOVUTI.
Reviewed by crispaseve
on
03:01
Rating:
Post a Comment