NAPE ABAINISHA SABABU ZA KUCHELEWA KWA VIKAO VYA CCM
KATIBU
wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye,
akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma leo asubuhi Julai 10, 2015.
Nape
amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba
kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo
yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11,
2015.
Nape
amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote
kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na
vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho
ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu.
Alipoulizwa
ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia,
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika
kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo
kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa
wakikutana kwa majadiliano na wadau kingawa hakueleza ni wadau gani.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi
wa habari nje ya Ukumbi wa White House, Mjini Dodoma leo Julai 10, 2015.
NAPE ABAINISHA SABABU ZA KUCHELEWA KWA VIKAO VYA CCM
Reviewed by crispaseve
on
04:59
Rating:
Post a Comment