TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services yafutulisha wadau wake
Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, kushoto, akitembelea
katika ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services katika
futuru iliyoandaliwa na taasisi hiyo. Pichani ni wadau wengine
walioalikwa katika futari hiyo.
TAASISI
ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imefuturisha wadau wake
wanaoendelea na mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, huku ikiwataka
kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote. Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala wa Bayport Financial Services,
Evelyine Hall, katika futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wadau wake
mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu
mbalimbali.
Viongozi wa
Taasisi ya Bayport Financial Services na wageni waalikwa wakijadiliana jambo
katika futari ya Bayport iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mwenye koti
jeusi na kofia ni Haruna Mbeyu, akifurahia jambo.
Akizungumza
katika futari hiyo, Evelyine alisema ni vyema Watanzania wote, hususan Waislamu
kuutumia vyema mwezi huo, ikiwa ni nguzo muhimu katika Dini ya Uislamu Tanzania
na duniani kwa ujumla. Alisema
Bayport inaheshimu misingi ya dini zote, hivyo kwakuwa mwezi wa Ramadhan ni
sehemu ya ibada kwa Waislamu, vyema wakautumia vizuri, sanjari na kulinda
Amani, upendo, umoja, mshikamano, bila kusahau jamii kuishi kwa kuheshimiana
ili nchi yetu iweze kupiga hatua.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza wa tatu kutoka
kulia, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Kifedha ya
Bayport Financial Services, mara baada ya kumaliza kufuturu katika
futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, huku ikiandaliwa na
Bayport.
Wakati wanatembelea katika ofisi ya taasisi hiyo baada ya kumaliza kupata futuru, jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega, mwenye kanzu akizungumza jambo
katika futuru iliyoandaliwa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial
Services, iliyofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, mwishoni mwa wiki,
jijini Dar es Salaam. Kulia kwa DC ni Meneja Utawala wa Bayport,
Evelyine Hall na anayemuhoji DC ni Mwandishi wa Habari, Phillip Daudi,
aliyeshika kipaza sauti. Picha na Mpiga Picha Wetu.
“Bayport Financial Services inajivunia kutoa huduma kwa Watanzania
wote, ambao leo baadhi yao wapo katika ibada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa
Ramadhan, hivyo tunaamini mwezi huu utakuwa na tija, endapo utatumiwa vyema,”
alisema Evelyine.
Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services,
Ngula Cheyo, alisema kuwa Watanzania wamekuwa wakiishi kwa kuheshimiana, hivyo
wanaamini wataendelea kutoa huduma bora ya mikopo ya fedha, mikopo ya viwanja,
mikopo ya bidhaa mbalimbali kama vile injini ya boti, vifaa vya ujenzi, ambapo
huduma zote hizo zinapatikana kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz na kupitia mawakala na ofisi zao
zilizoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara.
Mkuu
wa Wilaya Kilwa, DC Abdallah Ulega kulia, akipiga picha na Meneja
Utawala wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Evelyine
Hall na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services,
Ngula Cheyo kushoto. DC alikuwa miongoni mwa wadau walioalikwa katika
tukio la futari lililofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na
taasisi hiyo inayojihusisha na mambo ya mikopo.
Katika hatua
nyingine, Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdallah Ulega, aliipongeza Bayport kwa kitendo
chao cha kiungwana cha kuamua kuandaa futari hiyo kwa wadau wao. “Sisi serikali tutaendelea kuwaunga
mkono wadau mbalimbali wenye kuamua kuanzisha mambo mazuri kama haya, hivyo
tunawapongeza kwa dhati juu ya jambo hili muhimu linalojenga kuheshimiana kwa
namna moja ama nyingine,” alisema Ulega.
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services yafutulisha wadau wake
Reviewed by crispaseve
on
06:21
Rating:
Post a Comment