Header AD

Twanga Pepeta kufanya shoo kabambe Sikukuu ya Eid Mosi Giraffe Hotel

BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, inatarajia kufanya shoo kabambe Sikukuu ya Eid Mosi katika Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Aset Entertainment, Asha Baraka, alisema kuwa onyesho hilo litakwenda sambamba na utambulisho wa wimbo mpya wa mwanamuziki wao aliyerejea kundini hivi karibuni, Khalid Chokoraa unaokwenda kwa jina la Prison Love.
 
Alisema kwamba onyesho hilo ni maalum kwaajili ya kuwapa burudani mashabiki wao baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na kumkaribisha Chokoraa aliyerejea Twanga Pepeta akitokea Mapacha Watatu.
 
“Onyesho hilo litakuwa ni kwaajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wetu baada ya mfungo wa Ramadhani, tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwani kutakuwa na mambo mazuri ambayo ni ‘surprise’,” alisema Asha anayefahamika pia kwa jina la Iron Lady.
 
Kiongozi huyo alisema wanawasiliana na uongozi wa Giraffe Hoteli ili kuona kama wanaweza kutoa zawadi kwa mashabiki watakaopendeza zaidi na wanamuziki watakaopagawisah zaidi siku hiyo.
 
Wanamuziki wanaounda bendi hiyo kwa sasa wapo katika mazoezi makali kujiandaa na shoo hiyo chini ya uongozi wa wakongwe Ally Choki na Luiza Mbutu.
Twanga Pepeta kufanya shoo kabambe Sikukuu ya Eid Mosi Giraffe Hotel Twanga Pepeta kufanya shoo kabambe Sikukuu ya Eid Mosi Giraffe Hotel Reviewed by crispaseve on 03:32 Rating: 5

No comments

Post AD