MSIMU MPYA WA SOKA BARANI ULAYA WAZINDUA NA DSTV.
Mkurugenzi
wa Multichoice Maharage Chande katikati akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa soka barani Ulaya leo Jijini Dar es
salaam, kulia ni Meneja Uendeshaji Ronald Baraka Shelukindo na kushoto
ni Afisa Masoko Furaha Samalu.
Mkurugenzi
wa Multichoice Maharage Chande akimkabidhi mwandishi wa habari wa Kituo
cha TBC Evance Mhando dekoda ya DSTV leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa michezo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Multichoice Maharage Chande jijini Dar es Salaam leo.
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KAMPUNI
ya Multichoice Tanzania kupitia kisimbuzi cha DSTV kimezindua msimu
mpya wa soka barani Ulaya huku kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Uingereza
ikitangazwa kwa lugha ya kiswahili. Msimu huo mpya unaotarajiwa kuanza
Agosti 13 unat anatarajiwa kuwa wa kipekee hasa baada ya kupunguza bei
kwa watumiaji wapya ambapo watapata kwa dekoda kwa shilingi 79,000.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mwaka mpya wa Soka, Mkurugenzi wa Multichoice
Maharage Chande amesema kuwa msimu huu mpya utakuwa ni wa kipekee sana
kwani kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Uingereza itakuwa inatangazwa kwa
kiswahili ambapo watanzania wataweza kuelewa vizuri sana na hii itakuwa
ni muendelezo kama ilivyo ligi ya Hispania.
Chande
amesema kuwa watu mwaka huu watapata na nafasi ya kuangalia burudani ya
mpira na takribani mechi 300 zitakazonyeshwa moja kwa moja ambapo
SuperSport wataonyesha kupifia chaneli za SS3, SS5, SS6, SS7 na SS11 kwa
ligi kuu ya Uingereza huku ligi ya Hispania ikiwa ikionyeshwa kupitia
kifurushi cha DSTV Compact.
Meneja
Mauzo wa Multichoice, Baraka Shelukindo amesema kuwa mbali na kupungua
kwa bei hiyo, channeli zimeingizwa katika kifurushi cha 84,000 na pia
kwa sasa wapo kwenye mikakati ya kuandaa application mpya ya ya
SuperSport ambazo zitakuwa na live Streaming pamoja na video zilizojiri
za kuvutia.
Katika uzinduzi huo DSTV walichezesha droo na kuwapatia dekoda waandishi wanne wa habari.
MSIMU MPYA WA SOKA BARANI ULAYA WAZINDUA NA DSTV.
Reviewed by crispaseve
on
06:22
Rating:
Post a Comment