SUPER GIRLS BINGWA AIRTEL RISING STARS LINDI
Nahodha
wa timu ya Super Girls Tatu Makota akipokea kombe la ubingwa wa
michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi kutoka kwa Katibu Tawala
wa wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo baada ya kuifunga VC Vito Malaika
4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo akikagua timu wakati wa
fainali za michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi zilizofanyika
kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea. Super Girls ilishinda 4-1 dhidi ya
VC Vito Malaika.
Wachezaji
wa timu ya Super Girls wakishangalia ubingwa wa michuano ya Airtel
Rising Stars mkoa wa Lindi baada ya kuifunga VC Vito Malaika 4-1 katika
fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.
TIMU
ya wasichana ya Super Girls imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini
ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Mkoa wa Lindi baada ya
kuichapa FC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa
Sokoine mjini Nachingwea. Katika michuano hiyo, Mpiruka Queens iliweza
kuibuka mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kipara Queens 2-1.
Katika
mchezo wa fainali, Super Girls walianza kwa kasi na kuliandama lango la
wapinzani wao tangu dakika za mwanzo lakini ilibidi kusuburi hadi
dakika ya 15 ili kuandika goli la kwanza. Goli hilo lilofungwa kwa
ustadi na mchezaji Ashura Mfaume baada kungongeana vizuri na Tatu
Makota.
Baada
ya bao hilo, Super Girls waliendelea kutandaza kandanda safi na
kufanikiwa kufunga bao la pili dakika ya 18 lilifungwa tena na Ashura
Mfaume baada ya kuwalamba chenga mabeki watatu wa FC Vito Malaika. Bao
la tatu lilifungwa na Alia Fikiri mnamo dakika ya 22 baada ya mabeki wa
FC Vito kushindwa kuokoa mpira wa kona.
Timu
ya FC Vito Malaika walipata bao lao pekee katika dakika ya 27 baada ya
mchezaji Sarah Isaac kuachia shuti kali na mpira kujaa moja kwa moja
wavuni. Hadi mapumziko, Super Girls 3 FC Vito Malaika 1.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikasaka bao lakini ilikuwa ni
Super Girls waliopata goli dakika ya 63 baada ya mchezaji Tatu Makota
kufunga kwa penati baada ya beki wa FC Vito Malaika kunawa mpira kwenye
eneo ya hatari.
Akiongea
kwenye fainali wa michuano hiyo,mgeni rasmi Hadja Sekibo ambaye ni
Katibu Tawala wa mkoa wa Nachingwea aliwapongeza kampuni ya Airtel kwa
kuwekeza kwenye soka la wanawake nchini. ‘Nachukua nafasi ya kuwapongeza
wenzetu wa Airtel kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye soka vijana wetu
sana sana kwa wasichana.
Tunatambua
soka ni ajira, lakini kuwapa hawa vijana wetu wa kike nafasi ya
kuonyesha vipaji vyao, mnawafungulia milango ya kuonekana nchini nzima
na pia kunawafanya kutoweza kujiingiza kwenye makundi yenye malengo
mabaya kwani muda wao wa ziada wanatumia kucheza mpira. Kwa hivyo
wanapongeza kwa kuweza kuunga mkono jitihada za serikali za kuwawezesha
vijana kujiajiri’, alisema Sekibo.
Naye
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Lindi Ally Mkadeba
alisema michuano ya Airtel Rising Stars imewawezesha kupanua wingo wa
kutafuta vipaji vya soka mkoani na kufikia maeneo mengi ambayo bila
Airtel Rising Stars wasingeweza kufika. Mkadeba aliongeza kuwa wakati wa
michuano hiyo, makocha waliweza kuchangua wachezaji 16 ambao hana
uhakika kuwa watawakilisha vyema Mkoa wa Lindi kwenye fainali za
michuano hiyo ambazo zitafanyika Dar es Salaam kuanzia Septemba 6-11.
SUPER GIRLS BINGWA AIRTEL RISING STARS LINDI
Reviewed by crispaseve
on
06:37
Rating:
Post a Comment