ANDAENI WATAALAMU WA KUTOSHA- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitaza mashine ya CT Scanner wakati
alipotembelea na kukagua ujenzi wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya
na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es
salaam Septemba 2, 2016.




Ametoa
agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 2, 2016) wakati alipokagua maendeleo
ya mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na
Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha
Kimataifa cha Muhimbili katika eneo la Mloganzila.
Amesema Serikali zilizotangulia zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua nzuri ya kuongeza wataalam ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya.
Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia utawapunguzia wananchi adha ya kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu nje ya nchi. Tayari upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo umeanza kufanyika nchini.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Humphrey Polepole awasake watu wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za mafuta ya kuendeshea mitambo katika karakana ya mkandarasi anayejenga Kampasi hiyo.
“Wafanyakazi waache wizi. Lita 1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii kampuni inayolinda kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya usimhurumie mwizi,” amesisitiza. Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema kukamilika kwa kampasi ya Mloganzila kutasaidia upatikanaji wa madaktari bingwa wengi nchini ambao watapunguza gharama za kupeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Awali, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa hospitali pamoja na kampasi yote ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa wataalamu wa afya nchini.
Amesema hospitali hiyo itatumika kutoa huduma za afya za kitaalam zaidi kwa magonjwa mbalimbali, hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu. Pia itapunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ujenzi wa mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43. Kukamilika kwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila kutawezesha chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa fani ya afya kutoka 4,010 hadi 15,000.
Prof. Kaaya amesema mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ulisainiwa tarehe 12, Desemba, 2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2016.
ANDAENI WATAALAMU WA KUTOSHA- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
Reviewed by crispaseve
on
06:42
Rating:

Post a Comment