Airtel na VETA yatoa elimu juu ya masomo ya ufundi kupitia simu ya VSOMO
  Walimu na wanafunzi wa
 Chuo cha VETA Kipawa wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson 
Mmbando (kushoto) akifafanua juu ya ushirika kati ya Airtel na VETA kwa 
kuleta mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA
 kwa njia ya simu yajulikanayo kama Vsomo yaani VETA Somo, katika semina
 iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki 
iliyopita.
 Mkuu wa Chuo cha VETA 
Kipawa, Eng. Lucius Lutenganya akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi 
wa chuo hicho juu ya  programu ya Vsomo yaani VETA Somo inayotolewa na 
kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo
 wanafunzi wa Chuo cha VETA watapata fursa ya kusoma  kupitia simu za 
mkononi, kulia ni Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi na 
Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba. 
Semina hiyo
iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. 
 Meneja huduma kwa 
Jamii wa Airtel Hawa Bayumi (kulia) akielezea faida za programu ya VSOMO
 kwa walimu na wanafunzi wa chuo cha VETA Kipawa inayowezesha kupata 
mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya
 simu katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam
 mwishoni mwa wiki iliyopita. 
  Mratibu wa kozi fupi 
na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba akijibu swali juu ya kozi 
zipatikanazo kupitia program ya VSomo yaani VETA Somo inayowezesha 
kupata mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa
 njia ya simu, katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar 
es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Wanafunzi wa Chuo cha Veta Kipawa wakisikiliza kwa makini katika semina juu ya mpango wa VSomo yaani VETA Somo
inayowezesha kupata mafunzo ya ufundi stadi
 kutoka VETA kwa njia ya simu, ambapo wanafunzi wa VETA watapata fursa 
ya kusoma kwa kupitia simu za mkononi wakati wa semina iliyofanyika 
chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni
 mwa wiki iliyopita
Airtel na VETA yatoa elimu juu ya masomo ya ufundi kupitia simu ya VSOMO
 
                    Reviewed by crispaseve
                    on 
                    
01:50
 
                    Rating: 
                    
Post a Comment