MASHINDANO YA MEI MOSI KITAIFA YAZINDULIWA MJINI MOSHI
Timu
ya Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
wakiingia uwanjani kwa maandamano wakati wa uzinduzi wa mashindano ya
Mei Mosi kitaifa yanayofanyika mjini Moshi.
Timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiingia uwanjani .
Timu ya Wizara ya Uchukuzi wakingia uwanjani.
Timu
za Mashirika na Taasisi mbalimbali wakiwa wamebeba mabango wakati wa
ufunguzi rasmi wa mashindano ya Mei Mosi yanayofanyika kitaifa mjini
Moshi.
Katibu
Mkuu wa Kamati ya Mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Awadi Safari
akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo uliodfanyika
katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Kaimu
Mwenyekiti wa kamati ya Mashinano ya Mei Mosi Kitaifa ,Joyce Benjamini
akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo katika
uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Mgeni
rasmi katika ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ,Mkuu wa wilaya ya
Moshi,Kippi Warioba akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (aliyevaa suti) akiongozana na Kaimu
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Joyce Benjamin
kwa ajili ya ukaguzi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo.
Mwamuzi wa Kike ,Salma akimtamburisha Mkuu wa wilaya timu mbalimbali zilizopo pamoja na kumkaribisha kwa ajili ya ukaguzi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya RAS Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya Geita Gold Mining.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa Netiboli wa timu ya RAS Kilimanjaro.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi
wa mashindano ya Mei Mosi kitaifa yanayofanyika katika uwanja wa Chuo
Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Timu ya soka ya Geita Gold Mining wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya RAS -Kilimanjaro .
Timu
ya soka ya RAS -Kilimanjaro kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya
kuanza mchezo wake dhidi ya Geita Gold Mining ,mchezo ulimalizika kwa
timu ya RAS-Kilimanjaro kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.
Kikosi cha timu ya TPDC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wake dhidi ya timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Kikosi
cha timu ya Halmashari ya wilaya ya Hai kikiwa katika picha ya pamoja
kabla ya mchezo wake dhidi ya TPDC mchezo uliomalizika kwa TPDC
kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.
Mshambuliaji
Tumaini Masue wa timu ya Chuo Kiku cha Ushirika Moshi,akijaribu kumpita
mlinzi wa timu ya RAS -Kilimanjaro mchezo ambao timu ya Ushirika
ilichomoza na ushindi wa bao 2-1.
Wachezaji wa timu ya TPDC na Halmashauri ya wilaya ya Hai,wakichuana vikali .
Mchezo mwingine ulikua ni netiboli ambapo ,timu zimekuwa zikichuana vikali kuwania umalkia wa mchezo huo.
Timu
za TPDC na MUHAS zikimenyana katika mchezo wa kuvuta Kamba ,mchezo
ulimalizika kwa TPDC kushinda mhezo huo baada ya kuwavuta wenzao kwa
awamu mbili.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
KAMATI
ya Mashindano ya Mei Mosi ,imeonya timu za Mashirika kutumia
wanamichezo wasio watumishi (Watumishi Bandia ) katika mashindano hayo
huku ikitangaza kutoa adhabu kali kwa taasisi ama mashirika
yatakayobainika kuwatumia wachezaji hao.
Kwa
mujibu wa kanuni za mashindano hayo ambayo hufanyika katikamkoa ambao
siku kuu ya Wanyakazi Duniani hufanyika kitaifa, timu zitakazo bainika
kufanya udanganyifu zitafikwa na rungu la kufungiwa mwaka mmoja
kutoshiriki mashindano hayo pamoja na faini ya kiasi cha sh 500,000.
Mbali
na adhabu hiyo kwa timu iliyofanya udanganyifu ,pia viongoz wa timu
husika watafungiwa kwa muda wa miaka miwili kushiriki mashindano ya Mei
mosi ,adhabu itakayoenda sambamba na nakala ya barua kwa waajili wa
viongozi hao ya kuonesha namna watumishi hao si waaminifu.
Katibu
Mkuu wa Kamati ya Mashindano hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo
Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCu) baada ya kuzinduliwa jana ,Hawad Safari
alisema ili kutoa uhakiki kamati imetoa maelekezo kwa wanamichezo wafike
na vitamburisho vya kazi,Fomu inayoonesha mshahara pamoja na kadi ya
bima ya afya.
Alisema
mashindano hayo yanahusisha timu kutoka katika mashirikisho manne
ambayo ni Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Uma (SHIMUTA),Shirikisho
la Michezo la Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI ) ,BAMATA
na Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
Safari
alisema hadi sasa jumla ya timu 14 kutoka taasisi na mashirika
mbalilimbali zimewasili mjini hapa kwa ajili ya kushindana katika
michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,Netiboli,Kuvuta kamba ,Mbio za
baiskeli ,Marathoni pamoja na michezo ya jadi kama Bao ,Drafti na
Karata.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo uliotanguliwa na maandamano
kwa timu shiriki,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba alisema zipo
taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa taasisi na mashirika wamezuia
kushiriki michezo hiyo licha ya kwamba timu zao zilikwisha fanya
maandalizi.
“Nivitake
vyama vyama vya wafanyakazi kufuatilia suala hili ,kwa nini wafanyakazi
hawashiriki katika michezo hasa hii ya Mei Mosi Kitaifa ….nchi yetu
imekuwa haipigi hatua kwenye eneo hili ni kwa sababu ya viongozi hawa
wasiopenda michezo mahala pa kazi”alisema Warioba.
Awali
akitoa hotuba yake Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo Joyce
Benjamini alisema Mashindano hayo yamelenga kuongeza ushirikiano mwema
kwa wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi huku akitoa rai kwa viongozi
kutenga bajeti kwa ajili ya mashindano hayo.
Timu
zinazo shiriki mashindano hayo ni pamoja na Wizara ya Uchukuzi,Mamlaka
ya Ustawishaji Makao Makao –CDA Dodoma,Ofisi ya Rais Ikulu,Shirika la
Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Timu
nyingine ni Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU),Halimashauri ya wilaya
ya Hai,Halmahauri ya wilaya ya Moshi ,Halmashauri ya Manispaa ya
Moshi,Ofisi ya katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Geita Gold
Mining,Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro na TAMISEMI.
Katika
michezo ya awali timu ya soka ya TPDC ilifanikiwa kuchomoza na ushindi
baada ya kuiadhibu timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai kwa bao moja kwa
sifuri huku timu ya Chuo Kikuu cha Ushirika ikitakata mbele ya timu ya
Ras –Kilimanjaro kwa jumla ya ba 2 kwa 1.
MASHINDANO YA MEI MOSI KITAIFA YAZINDULIWA MJINI MOSHI
Reviewed by crispaseve
on
04:29
Rating:
Post a Comment