TV 1 YAJITOSA KUTAFUTA FEDHA ZA MASHINDANO UA TENIS YATAYOFANYIKA MEI NCHINI ITALY
Katibu
mkuu wa Chama cha Tennisi nchini , Irene Jackson Mwasanga akizungumza
na waandsihi wa habari juu ya mpango wa kuiwezesha timu ya mchezo wa
Tennisi kwa walemavu
Meneja
Masoko wa TV 1 Tanzania , Gllian Rugumamu akizungumza na waandishi wa
habari juu ya mpango wa T V 1 Kusaidia timu hiyo hili iweze kusafiri
kwenda Italy kushiriki mashindano ya Dunia.
Promotion
Meneja wa kituo cha radio cha Times Fm, Namiundu Ngutupari akizungumza
juu ya kituo hicho kujiingiza katika kusaidia kupatikana kwa fedha za
wachezaji hao kuwawezesha kufika nchini Italy katika mashindano ya Dunia
Meneja
Masoko wa kampuni ya bima ya Tanzania Management Insuarance ,Johnson
Wariko akizungumzia jinsi kampuni yake ilivyojipanaga kuwawekea bima
wachezaji hao ambao watasafiri kwenda nchini Italay
Mcheza Tenisi Vosta Piter akijaribu kurudisha mpira uliopigwa na mwenzie katika mazoezi ya mchezo huo katika Viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam mcheza Tennisi akiwa katika mazoezi ya kawaida katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam leo
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Timu ya Magongo ya Tennis inahitaji
milioni 120 ili kuweza kushiriki mashindano ya kimataifa yanayotarajia kutimua
vumbi Mei 1 hadi Mei 6 nchini Italy.
Akizungumza na waandishi habari
jijini Dar es Salaam, Rais wa timu hiyo,
Denis Makoi amesema kuwa hadi sasa wamepata dola 3500 ambazo dola 3000 zimetolewa na Kampuni ya TPS na dola 1500 zimetolewa na shirikisho la Tenis
la Kimataifa.
Amesema mashindano hayo ni mhimu kwa timu hiyo kwani wao ndio
mabingwa wa Afrika hivyo kushiriki kwao kutaongeza kuwa na uwezo na kuiletea
Taifa heshima ya mchezo huo.
Makoi amesema kuwa TV One wamejitoa
kuungana na katika kutafuta fedha hizo ili timu hiyo iweze kushiriki mashindano
hayo yatayoifanya Tanzania kuingia katika ramani mchezo wa Tenis.
Meneja wa Masoko wa TV 1, Gillian
Rugumamu amesema wamejitoa katika kuhamasisha watanzania kuchangia timu hiyo
ili iweze kushiriki mashindano hayo.
Gillian amesema kama chombo cha
habari wanawajibu wa kuhamasisha mchezo wa tenis kutokana na vjana kuwa na
uwezo wa mchezo huo.
Amewaomba watanzania kuchangia kwa
njia mbalimbali ikiwemo kwa M-Pesa kwa kuingiza namba 5590901 kwa Benki ya NIC
kwa fedha ya Kitanzania A/C No.2000021086
na dola za Kimarekani kwa akaunti A/C NO. 2000021094.
Mcheza Tenisi Vosta Piter akijaribu kurudisha mpira uliopigwa na mwenzie katika mazoezi ya mchezo huo katika Viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam mcheza Tennisi akiwa katika mazoezi ya kawaida katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam leo
TV 1 YAJITOSA KUTAFUTA FEDHA ZA MASHINDANO UA TENIS YATAYOFANYIKA MEI NCHINI ITALY
Reviewed by crispaseve
on
11:01
Rating:
Post a Comment