Header AD

Airtel yachangia Ujenzi wa Kituo cha Afya Pemba - Michenzani: Yatoa Vifaa vya Ujenzi vya Milioni 10/-

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa Saruji 143 kwa Sheha wa Michenzani  Mzee Abdalah Omari huko Pemba visiwani  ikiwa ni msaada wa Airtel kushirikiana na wananchi wa Tanzania visiawani kwaajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali  za maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa wiki. Wakwanza kulia ni sheha wa Stahabu-pemba bw haji Faki Kombo na kati ni Afisa Mipango wa Wilaya Mkoani Bw Omar Shehe Omari.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa Nondo 62 kwa Sheha wa Michenzani  Mzee Abdalah Omari huko Pemba visiwani  ikiwa ni msaada wa Airtel kushirikiana na wananchi wa Tanzania visiwani kwaajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali  za maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI.

*****************
 . Kituo hicho kitafaidisha zaidi ya watu 9,000 wa maeneo ya Bogoa, Shidi na  Michenzani
   
. Airtel yakabidhidhi Mabati 264,  Saruji 143, Nondo 62 na Mbao za kupau kituo cha Afya Michenzani
 
Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiana na jamii sehemu mbali mbali kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kisiwani pemba maeneo ya michenzani kitakachosaidia kutoa huduma maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI.

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa Airtel Zanzibar Bw Hagai Samson alisema “msaada huu wa Airtel kwa wakazi wa huku pemba hautaishia hapa , leo tumejitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika kumalizia ujenzi wa kituo hiki cha afya tukiwa na imani vikitumika kwa usahihi vitasaidia kuboresha huduma za afya katika maene ya Michenzani, Chokocho, Kizumgu, Kandandarani na Shidi.

Airtel Tanzania tunawashukuru sana wateja wetu mliopo pemba kwa kuwa ndio hasa wanaotuunganisha na jamii hii siku ya leo. Tunachojitolea hapa ni sehemu ya faida tunayoipata kila mnapozitumia huduma zetu zikiwepo kupiga na kupokea simu, Airtel money pamoja na huduma yetu ya Internet ya  3.75G.

Kwa upande wake Sheha wa Michenzani akipokea  msaada huo wa vifaa vya ujenzi wa kituo hicho cha Afya aliishukuru Airtel na kuwaomba wadau wengine wanaofanya biashara kisiwani huko kuiga mfano huo wa Airtel.

“ naishukuru sana Airtel kwa msaada wao huu, utatusaidia sana kukamilisha ujenzi wa  kituo hiki cha Afya hapa michenzani, tunaamini hii ni jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh, Ally M. Shein  ambae wiki moja iliopita aliweka jiwe la msingi katika kituo hichi na kuhimiza  ujenzi wa kituo hiki uende kwa kasi ili kusaidia kupunguza adha ya mrundikano wa wagonywa katika kituo kimoja kile cha Bogoa.

Nae Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkoani Omari Shehe Omari akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ujenzi wa kituo hicho cha Afya una lengo la kupunguza matatizo ya afya yanayoikabili jamii inayoishi maeneo hayo hasa kwa kuzingatia wakina mama na watoto.

“Ninaipongeza Airtel sana kwa kujitolea na kutusaidia kufikia malengo yetu ya Milenia, sisi tuna dhamira ya kuboresha Afya na elimu kwa pamoja, kila Skuli iwe na kituo cha Afya au kila Shehia  (Serikali ya Mtaa) iwe na kituo chake cha Afya.

Hivyo kwa msaaada huu utasaidia sana serikali yetu kutifika malengo yake kwamba pia michenzani watapata kituo chao hapa karibu.” Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ina mkakati wa kutoa misaada ya kijamii kwa kugusa sekta za mazingira, Elimu na Afya kwa  lengo la kuisaidia serikali na jamii kwa ujumla kupambana na changamoto mbalimbali .

Mwaka huu wa 2012 pia Airtel  imejipanga kuhakikisha jamii iliyopo pembezoni mwa nchi mbali na kupata huduma bora ya mawasiliano ikiwemo ile ya Airtel money pia itashiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ili kujenga vyema ushirikiano na jamii kama ilivyoshiriki kuboresha miundombinu ya Afya  Visiwani Zanzibar.
Reviewed by crispaseve on 09:29 Rating: 5

No comments

Post AD