Header AD

Waziri wa Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe Aongoza Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC Kusimamia Uchaguzi Wa Angola Leo

  Waziri wa nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe akiwahoji baadhi ya wapiga kura maoni yake kuhusu zoezi la kupiga kura
 Upiga kura ukiendelea nchini Angola Leo
  Waziri wa nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe(wa tatu kushoto) akiwahoji wasimamizi wa uchaguzi na mawakala wa vyama kuhusu zoezi la upigaji kura 
----
 Wananchi wa Angola leo wanafanya uchaguzi Mkuu wa pili tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Uchaguzi mkuu huo wa Wabunge na Rais unahusisha vyama 9 vya siasa. Vyama vikubwa ya siasa ni chama tawala MPLA na chama kikuu cha upinzani UNITA.

Tanzania inaongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi ya SADC chini ya uenyekiti wa Mhe Bernard K. Membe, Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC. Timu ya SADC inahusisha waangalizi 110 wa Uchaguzi kutoka nchi za SADC wakiweko 13 kutoka Tanzania.

Hadi sasa zoezi la upigaji kura limefanyika kwa amani na utulivu na watu wengi wamejitokeza kupiga kura katika jiji la Luanda na viunga vyake.
Reviewed by crispaseve on 09:33 Rating: 5

No comments

Post AD