Header AD

TAASISI YA HASSAN MAAJAR YAKABIDHI MADAWATI 680 MKOANI NJOMBE

Mgeni rasmi ambaye ni mkoa wa Njombe , Kapteni mstaafu Asery Msangi wa pili mstari wa pili kutoka kushoto akiwa amekaa na watoto kwenye madawati mara baada ya tafrija ya makabidhiano ya madawati 680 kutoka kwa Hassan Maajar Trust na Tigo, yalitolewa katika Shule ya msingi Ruhuji kwa wilaya za Njombe,Makete,Ludewa na Wangi’ngombe makabidhiano hayo  yalifanyika 22 Oktoba.
 Mgeni rasmi, Kapteni mstaafu Asery Msangi alikabidhi madawati kwa ma DC wa wilaya hizo tano na kuwashukuru Tigo na Hassan Maajar Trust (HMT)  kwa msaada huo wa  madawati iliyochangiwa na ‘Tigo Tuchange’ . Kutoka HMT alikuwepo Mkurugenzi Zena Maajar Tenga na Kutoka Tigo Meneja Mauzo mkoa wa Iringa Ladislaus Karlo 
Mkuu wa mkoa wa Njomba na Mgeni rasmi, Kapteni mstaafu Asery Msangi katikati akiangalia moja ya madawati 680 yaliyotolewa kama msaada kwa shule za mkoa huo, kulia ni Meneja Mauzo mkoa wa Iringa Ladislaus Karlo na kushoto ni Mkurugenzi  Hassan Maajar Trust Zena Maajar Tenga  na mmoja wa watoto wa shule hizo.
Wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya kukabidhiwa rasmi.
Wanafunzi wakicheza halaiki katikaafla hiyo wakati wa makabidhiano ya madawati 680 mkoani Njombe.
Wanafunzi wakifurahi msaada huo kwa kutambua kuwa ni muhimu sana kwao ili waweze kupata elimu bila usumbufu wa mahali pa kukaa.

Reviewed by crispaseve on 01:57 Rating: 5

No comments

Post AD