Header AD

TAIFA STARS YAWABAMIZA MABINGWA WA AFRIKA ZAMBIA 1-0

 Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza Mrisho Ngassa bada ya kuipatia Stars bao la kuongoza dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa leo kwenye Uwanja wa Tgaifa, Dar es Salaam.. Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
                                             Mashabiki wa Stars wakifuatilia mchezo huo. 
Mchezaji Mwinyi Kazimoto wa Taifa Stars akimtoka Sululan Phiri wa timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. (PICHA NA KASSIM MBAROUK)

Taifa Stars imetoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0 lililopatikana dakika ya 45 ya mchezo. Bao hilo limefungwa na Mrisho Ngassa, kwa shuti la mbali akimalizia pasi ya Mwinyi Kazi moto.

 Bao hilo la aina yake lililodumu hadi kipyenga cha mwisho, lilifungwa umbali mrefu ambalo liligonga nguzo ya goli na kutinga wavuni ni kutoka umbali wa kama mita 18 ya bao. 

Katika kipindi hicho kila timu iliweza kufanya mashambulizi makali lakini safu ya ushambuliaji ya Stars ilishindwa kujiamini kwa kupoteza mipira mingi iliyokuwa inaipata. 

Hata hivyo Zambia akuonesha sana makeke kama ilivyo kwa Stars kupitia kwa mchezaji wake Ngassa ambaye alikuwa akipoteza mpira mingi kwa kutokuwa makini na kuogopa ufanyiwa madhambi. 

Stars-Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Nyondani,Frank Domayo,Amir Kiemba,Salum Abubakar,Mrisho Ngassa,Mwinyi Kazimoto, Hamis Mcha/Simon Msuva. 

Zambia- Danny Munyao, Chintui Kapamba,Hichani Himonde,Chisamba Lungu,Jame Chamanga/Shadrack
Malambo,Christopher Katondo/Stoppila Sunzu,Felix Katongo,Nathan Sinkala/Evans Kangwa,Roderick Kabwe/Francis Kasonde na Issac Chansa.
Reviewed by crispaseve on 10:03 Rating: 5

No comments

Post AD