POULSEN ATUA BONDENI KUZIDODOSA IVORY COAST NA MOROCCO
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen (pichani) ameondoka leo mchana (Januari 18
mwaka huu) kwa ndege ya South African Airways kwenda Afrika Kusini kuzifuatilia
timu za Ivory Coast na Morocco zinazoshiriki Fainali za 29 za Mataifa ya Afrika
(AFCON) zinazoanza kesho (Januari 19 mwaka huu) nchini humo.
Ivory
Coast na Morocco ziko kundi moja na Tanzania (Taifa Stars) katika kinyang’anyiro
cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani
nchini Brazil.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na inayoshika nafasi ya pili
katika kundi hilo ambalo pia lina timu ya Gambia itacheza na Morocco, Machi 24
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Reviewed by crispaseve
on
09:32
Rating:
Post a Comment