fastjet yatoa mafunzo kwa Mtanzania wa Kwanza Mmaasai kuongoza ndege aina ya Airbus
Rubeni William Zelothe Stepehen akiwa mbele injini ya ndege aina ya Airbus A319punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet
Rubeni William Zelothe Stepehen akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319
Rubeni William Zelothe Stepehen akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet
Rubani William Zelothe Stepehen akiwa mbele ya ndege aina ya Airbus A319
William Zelothe Stepehen ni Mtanzania wa Kwanza Mmaasai aliyepewa ithibati ya kuiongoza ndege aina ya Airbus A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo hayo nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi nchini Tanzania hivi karibuni. William alikulia Olosipe jijini Arusha ambapo ni nyumbani kwa wazazi wake.
William
anafananisha anavyojihisi anapoiongoza ndege ya Airbus A319, na wakati
akiwa katika nyumba nzuri ya kifahari na ya kisasa; anaielezea ndege ya
Airbus A319 kama ndege iliyo imara na ambayo imewekewa mifumo mingi ya
usalama. Kwa maneno yake mwenyewe, anasema “Ndege ya Airbus inakulinda
kweli kweli, kama unaifahamu vyema”
William
amewahi kusomea usimamizi wa wanyama pori; alipata mafunzo ya urubani
kwa mara ya kwanza kule Florida Aviation Academy nchini Marekani mwaka
2006 ambapo alipata leseni yake ya usafirishaji kwa ndege. Ingawa ana
umri mdogo, ana uzoefu wa masaa 3,053 ya kuongoza ndege.
Kumwajiri
rubani huyu mtanzania mwenye miaka 28, ni mojawapo ya jitihada za
fastjet za kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaajiri watendaji wazawa
waliobobea katika fani hiyo hapa nchini. Mikakati yao ya kuajiri pia ni
mojawapo ya wajibu wao mpana wa kuwekeza nchini Tanzania. Kwa kila
rubani aliyepokea mafunzo, fastjet imetumia gharama inayokadiriwa
shilingi 49,546,400 hela za kitanzania ambayo ni sawa na 31,027 dola za
kimarekani.
fastjet
ni shirika jipya la ndege la nauli nafuu Afrika ambalo lilipata umiliki
wa FLY540 na kwa mantiki hiyo likazindua kampuni ya kwanza ya usafiri
wa ndege ambalo linazingatia bajeti. Fastjet, ambayo inaungwa mkono na
mwanzilishi wa Lonrho na easyGroup Bwana
Stelios Haji Ioannou, imetambulisha nauli za kiwango cha chini hadi
kiasi cha Tsh32,000 bila kujumlisha kodi ili kuwawezesha mamilioni ya
watu ambao walikuwa wameshindwa kusafiri kwa ndege, kuweza kusafiria
ndege kwa mara ya kwanza na kuendelea kutumia ndege mara kwa mara. Tangu
kuzinduliwa kwake mwezi Novemba 2012, shirika hili la fastjet
limewasafirisha zaidi ya watu 70,000 na asilimia 99.7 ya safari za ndege
zikisafiri katika muda uliopangwa.
Reviewed by crispaseve
on
03:46
Rating:
Post a Comment