MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA RASMI MRADI WA UPANUZI WA BARABARA YA KILWA, MBAGALA RANGI TATU
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati
alipowasili katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya
Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi,
Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza jambo na kumpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki
Okada, mara baada ya balozi huyo kumaliza kusoma hotuba yake
iliyochanganywa na Kiswahili, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa
Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Kushoto ni
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada,
akishiriki kucheza sebene la bendi ya Msondo Ngoma na Vijana wa kikundi
cha uhamasishaji cha Temeke, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa kutoa burudani wakati wa halfa hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakifunua kitambaa
kwa pamoja ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara
ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi,
Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, Waziri wa Ujenzi, Dkt.
John Pombe Magufuli na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kushoto)
wakishiriki kwa pamoja kukata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi
wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya Wazee wastaafu wa CCM, mara baada ya kumaliza
kupiga nao picha ya pamoja ya kumbukumbu wakati wa hafla ya ufunguzi wa
mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi kutembea na kukagua sehemu ya
Barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Rangi tatu, baada ya kufungua rasmi
barabara hiyo iliyokamilika kwa Upanuzi na ukarabati. Hafla hiyo ya
ufunguzi imefanyika leo. Picha na OMR
Reviewed by crispaseve
on
09:39
Rating:
Post a Comment