Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Tanga
Meneja Mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway akikabidhi baadhi ya vitabu vya sekondari kwa afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa ikiwa ni msaada ulitolewa kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila, anaeshuhudia wakwanza kulia ni Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga
Kulia ni Afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa ikimkabidhi kati ya vitabu vilivyotolewa kwa lengo la kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Mwishoni mwa wiki Airtel ilitoa vitabu kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila,. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga.
========== ======== =======
Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Tanga.
• Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu Tanga ni shule ya sekondari ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila
• Airtel yaahidi kuingia katika awamu mpya ya ugawaji wa vitabu kwa
sekondari kila mkoa nchini.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa vitabu
vya hesabu,chemistry na baologia vyenye thamani ya shilingi milioni 12
kwa shule nne za mkoa wa Tanga. Msaada
huo ni sehemu ya mpango wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wa
kusaidia ukuaji wa sekta ya limu kupitia kampeni yake ya shule yetu.
Akipokea
vitabu hvyo kwa niaba ya shule za mkoa wa tanga afisa elimu wa wilaya
ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa alisema, “ Tunawashukuru ziendelea katika shule mbalimbali mkoani hapa na mikoa mingine ya
Airtel kwa msaada huu wa vitabu kwani utasaidia kupunguza tatizo la
uhaba wa vitabu kwa shule zilizopatiwa msaada huo na kuongeza kiasi cha
ufaulu kwa wanafunzi. Tunaomba juhudi hizi zisihishie hapa Tanzania ili
kuondoa ujinga na umaskini na kuwapa watoto wetu elimu bora kwani hawa
ndio taifa la kesho.
Kwa
upande wake meneja mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro Bw.
Edmund Lasway amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni
yake wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini. Chini ya mpango maalumu wa
Shule yetu tumeweza kuzifikia shule nyingi za sekondari nchini.
Akiongea
kwa niaba za shule zilizopokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule ya
secondari ya Mkuzi juu Bwn Victor Mwenda alisema” Tunatoa
shukrani kwa Airtel kwa msaada wa vitabu katika shule zetu za sekondari,
kwa hatua hii itasaidia kupunguza tatizo la vitabu linalozikabili na
kuongeza ufanisi katika masomo ya sayansi. Tunawaomba wanafunzi
wavitunze na kuvitumia vizuri hivi vitabu kwani ni nyenzo muhimu katika
elimu ya sekondari.
Vilevile
Meneja wa huduma za jamii wa Airtel Tanzania Bi Hawa Bayuni alidokeza
kuwa Airtel iko katika mkakati wa kuanza awamu nyingine ya
ugawaji wa vitabu kwa shule za sekondari kwenye kila mkoa ikiwa ni
program yake ya mwaka huu ya kurudisha kwa jamii kupitia elimu
“tunaingia katika awamu ya mpya ya utowaji wa vitabu kwa shule nyingi
zaidi kila mkoa hapa Tanzania, mradi wetu huu utazingatia zaidi shule
za sekondari zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu kwamba ni shule zipi
zina uhitaji mkubwa wa vitabu na kushauri ziingie katika mpango wa
kusaidia jamii wa Airtel shule yetu” alieleza Bayumi.
Airtel
toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka nane iliyopita tumeweza
kuzifikia zaidi ya shule 1500 za sekondari zilizopo Tanzania kila
kona ya Tanzania na pia kukarabati miundombinu ya shule kwenye kwa
kutoa msaada sawa kwa mikoa yote na kuwafikia wanafunzi katika maeneo
mbalimbali hapa nchini ikiwa ni hatua ya Airtel kukuza kiwango cha elimu
kwenye maeneo mbalimbali Tanzania aliongeza Bayumi.
Shule
zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi mkoa ni Tanga ni pamoja na shule
ya sekondari ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila.
mkakati ni kuendelea kutoa vitabu kwa shule mbalimbali nchini ambapo
droo ya shule za sekondari zitakazo faidika na vitabu kwa mwaka huu wa
2013 -2014 itafanyika mwenzi Juni na kutoa nafasi kwa shule nyingine
nyingi za sekondari nazo kufaidika na mpango huu wa Airtel shule yetu.

Post a Comment