PICHA ZA TAMASHA LA DR.JOSE CHAMELEONE ‘TUBONGE 2014 LIVE CONCERT’ LILOFANYIKA NCHINI UGANDA.
Baada ya kusubiriwa kwa kipindi kirefu, hatimaye tamasha
kubwa la Tubonge liloandaliwa na msanii nguli wa muziki kutoka nchini
Uganda, Dr.Jose Chameleone limeacha historia hapo jana katika viwanja
vya ‘Lugogo Cricket Oval’ na kuhudhuriwa na umati wa watu licha ya mvua
kubwa iliyokuwa ikinyesha .
Msanii kutoka Tanzania, Khaleed Mohamed ‘ T.I.D Mnyama’
alikuwa miongoni mwa wageni walihudhuria tamasha hilo kubwa ambalo pia
liliwapa nafasi wasanii nchini humo kukonga nyoyo za mashabiki akiwemo
Bobi Wine, kaka wa Chameleone, Ak47, kundi la GoodLyfe linaloundwa na
Weasle na Radio, David Lutaalo, Xess Kayemba, Kenzo na wasanii chipukizi waliopo kwenye lebo yake ya Leone Island, Diziza, Diziza VIP na wengine kibao .
PICHA ZA TAMASHA LA DR.JOSE CHAMELEONE ‘TUBONGE 2014 LIVE CONCERT’ LILOFANYIKA NCHINI UGANDA.
Reviewed by crispaseve
on
16:16
Rating:
Post a Comment