Bomu laripuka katika kanisa Katoliki Olasiti Arusha, wakati wa uzinduzi wa Parokia.

Kanisa katoliki parokia ya Olasiti ambalo leo hii lilikuwa linapandishwa hadhi na kuwa Parokia limelipuliwa na kitu kinachosemekana kuwa ni bomu, watu wengi wamejeruhiwa na mtu mmoja inasemekana amefariki dunia.
Tukio hilo limetokea wakati Misa ikiwa ndio inaanza .Ilikuwa ni saa 5
kamili…Kabla Askofu hajaanzisha sala , mlipuko mkubwa ulitokea ndani ya
kanisa hilo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni balozi wa Vatican nchini Tanzania. Source: http://pamojapure.blogspot.com/
Ufuatao ni mkusanyiko wa habari hii kutoka vyanzo mbalimbali:
HABARI kutoka jijini Arusha zinasema kuwa kuna bomu limeripuka katika
Kanisa la Parokia Mpya ya Olasiti na kuzua taharuki ya aina yake.
Habari zinasema kuwa Kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa leo wakati
waumini kanisa hilo walikuwa wakiendelea na sherehe zao za uzinduzi huo,
huku lishangaza watu wengi, ingawa haijajulikana madhara ya mripuko
huo.
Taarifa za awali zinasema kuwa kuna gari lilifika hapo na kushuka mtu
ambaye baadaye bomu hilo lilisikika likiripuka na kuleta mkanganyiko
kwa waumini waliokwenda kufanya uzinduzi huo wa Kanisa. handenikwetu.blogspot.com
BOMU limelipuka kwenye uzinduzi wa kanisa la parokia mpya ya Yoseph
Olasiti mjini Arusha, ambapo Balozi wa papa alikuwa mgeni rasmi na
wageni wengi kutoka nje ya nchi, baadhi ya watu wameumia lakini hakuna
aliyepoteza maisha hadi hivi sasa na Polisi wamefika eneo la tukio.
Source: Kalulunga
Hali inakuwa tete katika nchi yetu Kanisani Parokia ya Olasit
kumetokea mlipuko haijajulikana kama ni bomu au la ila watu wamejruhiwa
inasikitisha. Source: Radio Maria via JF
Ukiwa Arusha tune FM 106.70
Nukuu kutoka Redio Maria
- watu wengi wamejeruhiwa miguu
- Olasiti Arusha
- kitu kilirushwa au kutokea chini kwenye moramu iliyo mwagwa….
- kuna watu wanahisiwa kuja eneo la tukio kwa gari na kurusha hiko kitu na kukimbia kutokomea na gari…maelezo ya mtoto mdogo anaye sadikiwa kuona watuhumiwa….
UPDATE:
…..mlipuko ulitokea katikati ya watu…..
….eneo limetapakaa damu….inasikitisha sana….
….niwakati Baba askofu akibariki maji ya baraka wakati anaweka chumvi ndani ya hayo maji (tendo la kubariki maji)..ghafra mlipuko ukatokea karikati ya watu….
….watu wako katika hali ya majonzi na masikitiko makubwa…..
Source: Earthmover, JamiiForums
Post a Comment