Header AD

DC MAKETE AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUWAPA ELIMU WANANCHI JUU YA HIFADHI YA MLIMA RUNGWE

DC Makete Bi,  Josephine Matiro
.................................................................................................
Na Esther Macha, mbeya

MKUU wa wilaya ya Makete Josephine Matiro amewataka viongozi wa kisiasa kuanzia ngazi za vijiji,kata,na tarafa na kutoka wilaya zinazo zunguka hifadhi za Kitulo, Eneo tengefu la Kipengere na Hifadhi ya Mlima Rungwe kuwaelimisha wananchi wao umuhimu wa hifadhi hizo badala ya kuendelea kulumbana juu ya mipaka ya harali ya hifadhi na mashamba ya wananchi.

Wito huo mumetolewa hivi karibuni na Mkuu huyo wa wilaya wakati akifungua warsha hiyo kwa viongozi wa kata amabo ni madiwani na maafisa watenaji,na tarafa pia na wataalamu wanao simamamia hifadhi hizo zinazo zunguka hifadhi hizo iliyofanyika katika Ukumbi wa FEMA unao milikiwa na kanisa KKKT Dayosisi Kusini Magharibi usharika wa Matamba wilayani Makete.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wanasiasa kuwa ahidi wananchi kwamba maeneo yalichukuliwa na hifadhi jizo yatarudishwa kwa wananchi kitu apacho hakipo na hakiwezekani kwani meneo hayo yametengegwa kwa mujibu wa sheria pia ni agizo kutoka kwa Rais hivyo hakuna kiongozi ambaye anaweza kutengea agizo hilo.

Alisema kuwa ni wakati sasa kwa viongozi hao wa siasa wakiwemo madiwani na wabunge wanatoka katika maeneo ya hifadhi na tengefu kutoa elimu kwa wananchi faida zitokana nazo na umuhimu wa hifadhi hizo kwa jamii hiyo inayo zunguka badala ya kuendelea kulumbana na wataalamu walioajiliwa na serikali kwa ajili ya kusimammia hifadhi hizo.

“Ndugu zangu vingozi wa kata na tarafa pamoja na hasa nyie madiwani msiwadanganye wananchi kwamba eti maeneo yaliyo tengwa yanaweza kurudishwa hilo halipo kwani ni hifadhi chache ambazo wananchi wake wanarusiwa kufanya shughuli zao ndani ya hifadhi lakini hapa kwetu hakuna kitu kama hicho kwa hiyo mkawambia wananchi hilo haliwezekana,pia tumienu mikutano ya hadhara ya kuwaleza wananchi faida zitokano uwepo wa hifadhi hizo” alisema Matiro

Alisema kuwa sehemu nyingi alizo pita na kusilikiza malalamiko ya wananchi wengi hawaja elezwa ukweli na elimu ya kutosha juu faida za kuifadhi mazingira na uwepo wa hifadhi hivyo amewataka viongozi hao kwenda kuwa elimisha wananchi ili kujenga mahusinano mazuri katika hifadhi na wananchi wano zunguka maneo hayo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa Duniani (UNDP) kupitia mratibu mradi wa kuboresha Mtandao maeneo yaliyo hifadhiwa kusini mwa Tanzania (SPANETS) Godwell Ole Meing’ataki ambao miongoni mwa waaandaaji wa warsha hiyo alisema kuwa lengo la kuwaita viongozi hao wa kisiasa ni kutaka kujadili kwa pamoja na kuondoa migogoro ambayo kimsingi haina tija kwa taifa.

Alisema sababu nyingine ya kufanya warsha hiyo kujadili kwa pamoja na viongozi hao ilikuibua miradi itakayo nufaisha wananchi wanao zunguka katika hifadhi hizo kama jamii zingine ambazo zipo karibu na maeneo ya hifadhi zinavyo nufaika.

Alisema kuwa hifadhi ya za Kitulo,Kipengere, na Mlima Rungwe ni hifadhi tegemezi na haziwezi kujiendesha zenyewe na zinategemea bajeti kutoka hifadhi zingine hivyo wameamua kuitisha warsha kuyatangaza maeneo hayo kiutalii ili yaweze kujitegemea na hatimaye yaweze kuwahudumia wana jamii wanao zunguka maeneo hayo.

Godwell alisema kuwa elimu inahitajika kwa jamii na nguvu zinahitajika kwa kutangaza vivutio vya utalii hasa kwa ukanda huu wa nyanda kusini ambako inaonekana haujaeleweka kikamililifu ili kuweza kuongeza kipata kwa jamii na hifadhi zenyewe.

Kwa upande wake mhifadhi Mkuu wa Mbuga kitulo Deus Mzimba ambao ndo wenyeji ni waandaaji wa warsha hiyo alisema kuwa vingozi wa kisiasa kuanzia wenyeviti wa vitongoji,vijiji,wakitumiwa wanaweza kupepusha migogro hiyo kwana imekuwa ikinzia ngazi ya vitongoji.

Mbali na hilo Mzimba alisema serikali kwa kushirikana na vingozi hao wana wajibu kutoa elimu ya ujasilimali kwa wananchi wanao zunguka maeneo hao ili wanapo kuja watalii waweze kupata huduma kwa urahisi.

Warsha hiyo ilianza jana na ilitajiwa kumalizika leo ikiwa imefanyika kwa siku mbili washiriki wa warsha hiyo ni madiwani,watendaji wa kata,na makatibu tarafa kutoka wilaya Makete,Njombe kwa Mkoa wa Njombe na Halmashauri za Mbeya Rungwe na Busokelo kutoka Mkoa wa Mbeya na watalaamu wa hifadhi kuoka Mlima Rungwe, Kitulo na Kipengele amapo wanatarajiwa kutoka na maazimio,na mapendekezo ya pamoja ili kuondokana na migogoro inayotokea katika hifadhi hizo.
Mwisho.
Reviewed by crispaseve on 10:09 Rating: 5

No comments

Post AD